KALA JEREMIA ASEMA BAADA YA KUFA KANUMBA BONGO MOVIE IMEYUMBA SANA

Msanii wa Hip-Hop Tanzania KALA JEREMIAH
Ikiwa Leo ni Siku ya kumbukumbu ya Kifo cha Hayati Sheikh Amri Abeid Karume Muasisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba na Mmmoja wa Waasisi wa Taifa La Tanzania Siku ambayo imekuwa Sambamba na Kumbukumbu ya Kifo cha Marehemu Steven Kanumba aliyekuwa Muigizaji Nchini Tanzania Kala Jeremiah @kalajeremiah ameamua Kufunguka Mengi Kuhusu watu hawa Wawili.
Akizungumza na @DjHaazu Kupitia Kipindi Cha DUNDO LA MAMBO JAMBO RADIO, Kala Jeremiah amemzungumzia Hayati Karume kama Mwanamapinduzi aliyewahi Kutokea na Kuikomboa Zanziba na Kutokana na Hekima zake alizokuwa amejaaliwa na Mungu aliona umuhimu wa Kuwapigania Wazanzibari wenzake kwa kupigana Vita na unyanyasaji na Utawala wa Kimwinyi ulikuwepo Zanzibar. Amesema Watanzania kwa Ujumla Tuitumie siku hii kwa Vitendo kwa Kupinga Manyanyaso yote na ubadhilifu unaofanywa na baadhi ya Viongozi wa Serikali ya Jamuhuri ya TZ ikiwa ni pamoja na Kujitokeza katika Kujiandikisha na Mwisho Kupiga Kura mwaka huu 2015 kwa ajili ya kuchagua Viongozi WELEDI.
Hakuishia Kumzingumzia Karume pekee bali amemzungumzia Pia aliyekuwa Nguli wa BONGO MOVIE Steven ambaye naye alitutoka Siku kama ya Leo Mwaka 2012 kwa kusema kuwa Kanumba alikuwa ni Msanii Mpambanaji aliyeipambania Sanaa Ya Filamu Nchini Tanzania na Tokea Afariki Dunia Tasnia ya Filamu Tanzania Imeyumba sana.
Kala Jeremiah anathamini sana Mchango wa Sheikh Karume na Mchango wa Steven Kanumba MSIKILIZE AKIZUNGUMZA KWA KU-CLICK LINK HII Inline imagehttps://www.hulkshare.com/r9fdu8530lxc  
karume
Hayati Abeid Aman Karume

Hakika Itakumbukwa na Kuheshimiwa Historia Iliyoachwa na Hayati Abeid Aman Karume aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar ambaye  Alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi.
Karume aliongoza mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hapo mwaka 1964. Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere. Baada ya muungano wa nchi hizi mbili uliozaa jina la Tanzania, Karume alikuwa makamu wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hatosahaulika Pia Mpambanaji wa Tasnia ya Filamu nchini Tanzania Steven Kanumba
Steven-Kanumba-425x600
Steven Charles Kanumba alizaliwa tarehe 8 Januari 1984Shinyanga -na alifariki tarehe 7 Aprili 2012 alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania. Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.

Post a Comment

أحدث أقدم