Polisi wakabiliana na waandamanaji nchini Burundi kufuatia tangazo la rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu wa urais.
Mbunge
wa zamani katika bunge la Afrika mashariki Francois Bizimana
ameripotiwa kutekwa nyara siku ya jumapili mjini Bujumbura na watu
wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na serikali.
Bizimana ni miongoni mwa viongozi wa upinzani nchini Burundi ambao wanampinga rais Pierre Nkurunziza.
Mwandishi
wa BBC Robert Kiptoo anasema kuwa vyombo vya habari vinaripoti kuwa
kiongozi huyo wa upinzani alitekwa na watu waliojihami.
Washirika wake pia wamekamatwa.
Post a Comment