Mwenyekiti
wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo
vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na maadhimisho ya siku ya
uhuru wa habari duniani (WPFD) yatakayofanyika tarehe 2 mwezi Mei mwaka
huu mkoani Morogoro.
Wanahabari
na wadau wa habari wanatarajiwa kukutana Mkoani Morogoro kwa siku
mbili kwa kusanyiko la maadhimisho ya siku ya Uhuru wa habari duniani
(WPFD), litakalofanyika katika hoteli ya Nasheera, Mjini Morogoro.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of
Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika), Ndugu
Simon Berege alieleza kuwa, kusanyiko hilo la wandishi wa habari na
wadau wa habari litafanyika mjini humo Mei 2-3, mwaka huu.
“Hii
ni mara ya kwanza WPFD kuadhimishwa mkoani Morogoro na mwakani
itafanyika mkoa mwingine nia ni kufanya kila mkoa kupata nafasi ya
kuadhimisha siku hiyo.
Wakati
wa maadhimisho hayo wadau watakumbuka gharama za waandishi wa habari
kukusanya taarifa mbalimbali na kuwapatia wananchi, gharama ambazo
wakati mwingine ni uhai wao au hata kunyimwa uhuru’ alieleza Berege.
Aidha siku hiyo watakumbukwa wale waliopoteza maisha kutokana na harakati za kutafuta habari kwa ajili ya umma.
Siku
ya WPFD, ambayo huadhimishwa duniani kote kila mwaka ilianzishwa na
Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuadhimisha kanuni za uhuru wa habari na
kuwakumbuka wale waliokufa wakijaribu kutekeleza kanuni hizo.
Kwa
maneno mengine WPFD ni jukwaa linalotumika na waandishi wa habari na
wadau wengine katika kutoa kauli za kushawishi serikali mbalimbali
kutunga sheria rafiki za vyombo vya habari ambazo zitahakikisha uwapo wa
uhuru wa habari.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Usalama wa habari katika ulimwenguj wa dijiti: Uandishi bora, Usawa wa jinsia na faragha’.
Berege
alibainisha kuwa, kwa kuzingatia kauli mbiu hiyo, WPFD 2015 itaangalia
masuala matatu muhimu: Ikiwemo Uandishi bora na ulio huru katika dunia
ya dijiti. Humu itajadiliwa uwingi wa vyombo vya habari na athari zake
katika majukumu ya uandishi na uwajibikaji kwa umma, masuala ya
kujiwabisha wenyewe, changamoto katika habari za uchunguzi, kauli za
uchochezi na vyombo vya habari na mafunzo ya habari.
Pia
suala lingine ni juu ya Wanawake na menejimenti ya vyombo vya habari;
na namna vyombo vya habari vinavyomuona mwanamke huku la mwisho likiwa
ni suala la Usalama wa waandishi wa habari hasa katika maeneo yenye
vurugu na jinsi ya kuhami vyanzo vya habari dhidi ya ufichuaji wa
kidijiti.
Katika
kongamano hilo pia litatoa nafasi ya kujadili na kutoa maazimio kuhusu
sheria zilizopitishwa na bunge na zile ambazo zimetamkwa kwa mara ya
kwanza. Sheria hizo ni pamoja na za Cybercrime Act, Statistics Act,
Media Services Bill and the Access to Information Law.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa, Wakati wa kongamano hilo walioathirika kwa kuvunjwa kwa uhuru wa habari watatoa ushuhuda wao.
Pia taarifa ya hali ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika iliyoandaliwa na MISA itazinduliwa rasmi.
Aidha,
katika tukio hilo, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez huku wadau
zaidi ya 200 wakiwemo wadau wa habari na maendeleo pamoja na
wawakilishi kutoka serikalini na mashirika mbalimbali ya kimataifa,
mabalozi, wabunge, vyama vya kijamii, asasi zisizokuwa za kiserikali,
waandishi maveterani,wakuu wa vyuo vya habari na waandishi wa habari.
Tukio
hilo limeandaliwa kwa pamoja na Media Institute of Southern
Africa-Tanzania Chapter [MISA (T) Chapter], Media Council of Tanzania
[MCT], Tanzania Media Fund [TMF], Union of Tanzania Press Clubs [UTPC],
United Nations Tanzania Office, UNESCO.
Wengine
ni Konrad-Adenauer-Stiftung Tanzania [KAS], Media Owners Association of
Tanzania [MOAT], Tanzania Editors’ Forum [TEF], Tanzania Media Women’s
Association [TAMWA), Morogoro Press Club na Tanzania Communication
Regulatory Authority [TCRA).
Aidha
kamati ya maandalizi ya WPFD 2015 imewezesha tukio hilo kwa
kushirikisha pia Government Employees Pensions Fund [GEPF], Alliance One
Tanzania, IPP Group of Companies, European Union (EU) na Tanzania
National Parks [TANAPA].
Mkurugenzi
wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) ambao ni miongoni mwa
wadau wa maandalizi ya maadhimisho hayo Bw. Ernest Sungura akifafanua
jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika
katika hoteli ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam leo. Kulia Mwakilishi
wa Umoja wa Mataifa ambao ni miongoni mwa wadhamini wa maadhimisho
hayo, Usia Nkhoma Ledama.
Makamu
Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waancdishi wa habari nchini (UTPC), Jane
Mihanji akisisitiza umuhimu wa wanahabari kuhudhuria maadhimisho ya siku
ya uhuru wa habari duniani (WPFD) ambayo kitaifa yanatarajiwa kufanyika
mkoani Morogoro Mei 2 mwaka huu. Katikati ni Mwakilishi wa Umoja wa
Mataifa ambao ni miongoni mwa wadhamini wa maadhimisho hayo, Usia Nkhoma
Ledama na kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania
(TMF) ambao ni miongoni mwa wadau wa maandalizi ya maadhimisho hayo Bw.
Ernest Sungura.
Miongoni
mwa wadau wa maandalizi ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari
duniani (WPFD) Bw.Richard Shaba kutoka KAS Tanzania na Mwakilishi kutoka
TAMWA, Godrida Jola wakisikiliza maswali kutoka kwa wanahabari (hawapo
pichani).
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini waliohudhuria mkutano huo.
Post a Comment