HII kali! Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Alice May
John (55) ameilalamikia nyumba yake iliyopo Sinza ‘D’ (Madukani)
wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam kwamba, ina mauzauza ya kutisha,
hali inayowafanya wapangaji kuikimbia kila wakati kwa kuhofia maisha
yao.
Alice May John anayelalamikia nyumba yake iliyopo Sinza ‘D’ (Madukani) kuwa na mauzauza.
Akizungumza na Uwazi hivi karibuni nyumbani kwake, Alice
alisema amekuwa akibanwa na wapangaji awarudishie kodi zao ili watafute
nyumba nyingine kutokana na kelele zinazosadikiwa ni za binadamu lakini
hawaonekani.
...wakiwa nje ya nyumba hiyo na mwandishi wa Global Publishers.
“Wakati nahamia hapa mwaka 2004 kutokea Mabibo (Dar) nilikorofishana
na mzee mmoja akanitishia maisha kwa kuniambia nitaona na ndipo majitu
hayo yakaanza kupiga kelele ya kulia usiku au mchana, wanalia hiiiii,
hiiii, hiiii! Unaweza kusikia kutokea chumbani, ukiingia huoni mtu.
“Nimechoka kurudisha fedha kwa wapangaji, mimi nategemea nyumba hii kupata pesa za kuendeshea maisha yangu.
“Wakati fulani nashindwa kuwarudishia fedha kwani nakuwa
nimeshazitumia na hapo ndiyo mgogoro unapoanza, wapangaji wengine
huondoka hata bila kunidai wakiamini mimi ndiye nashirikiana na hayo
majitu.
Akisimulia muda wa sauti hizo kuanza, mwanamke huyo alisema: “Mara
nyingi huanza saa 12 jioni wapangaji wanapoanza kuingia bafuni kuoga.
Kwa kweli napata tabu na nyumba yangu.
“Wapangaji wanaogopa, hawalali usiku kwani wakati fulani husikika
sauti kama ya bundi huku moto mkali ukionekana ukiwaka bila chanzo chake
kujulikana.
“Sasa hivi nimebaki na mpangaji mmoja tu ambaye si kwamba jasiri bali
anasubiri nimrudishie fedha zake. Nimechoka na haya majitu, sasa niende
wapi au nifanyeje? Siwezi kuikimbia nyumba yangu.
“Nilishakwenda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama
‘Mabatini’ (Dar) lakini wakasema wao hawawezi kushughulika na kesi ya
mauzauza.
“Siku nyingine nikaenda kwa mjumbe wangu, Peter Sabato Sanju wa Shina
Namba 7, Tawi la Sinza ‘D’ naye alisema hawezi kushughulika na watu
wasioonekana. Nimehangaika hadi makanisani nako sijaona tofauti.
Mjumbe Sanju alipohojiwa na Uwazi alikiri kupokea malalamiko
hayo kutoka kwa mama huyo lakini alishindwa kuyashughulikia madudu hayo
kwa sababu hayaonekani hivyo alimshauri aende kanisani kwa ajili ya
maombi.
“Ni kweli aliwahi kuja kuniambia, lakini tatizo ni kwamba, sauti za
ajabu zinasikika lakini huoni watu wala kitu, nikamwambia aende kanisani
akaombewe,” alisema mjumbe huyo.
Post a Comment