Dada mmoja aliyefahamika kwa jina la Jamila mkazi wa Kawe jijini Dar
hivi karibuni alipata kipigo cha kufa mtu akituhumiwa kuchepuka na mume
wa mwanamke mmoja aitwaye Sheila.Tukio hilo lilitokea hivi karibuni
ambapo ilielezwa kuwa, Sheila alitonywa na wambeya kuwa Jamila amekuwa
akichepuka na mumewe na bila kuchunguza akapanga kumshikisha adabu.
Jamila akiwa na jeraha usoni kwa tuhuma zakutembea na mume wa mtu.
“Jamila alikuwa akituhumiwa kutembea na mume wa Sheila na siku ya
tukio alifuatwa baa na kupigwa hadi kutaka kutobolewa jicho,” kilidai
chanzo.
Mwandishi wetu alifanya jitihada za kuwatafuta wahusika ambapo Jamila alipopatikana alisema:
“Jamani ukweli ni kwamba mimi niliwahi kutembea na yule mume wa Sheila lakini tulishaachana sasa nimemshangaa mkewe kuja na kunipa kipigo sababu tu ya maneno ya kusikia”, alisema Jamila na kuongeza:
“Jamani ukweli ni kwamba mimi niliwahi kutembea na yule mume wa Sheila lakini tulishaachana sasa nimemshangaa mkewe kuja na kunipa kipigo sababu tu ya maneno ya kusikia”, alisema Jamila na kuongeza:
Mwenye mume.
“Nilikwenda kufungua kesi Kituo cha Polisi Kawe lakini siku chache
baadaye Sheila alikuja na kuniomba msamaha akidai kuwa alikosea kuamini
maneno ya watu bila kufanya uchunguzi. Tumesameheana na yameisha.”
إرسال تعليق