Mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mtoto Nasra Mvungi,
Mariam Saidi akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi wakati akirudishwa
katika chumba cha mahabasu mara baada ya kusikiliza kesi inamkabiri ya
mauaji ambapo kesi hiyo sasa itasikilizwa katika mahakama kuu kanda ya
Dar es Salaam.Picha Juma Mtanda.
Juma Mtanda na Pascalina Kidyalla.
Rashidi
Mvungi baba wa Marehemu Nasra Mvungi ameondolewa katika shtaka la
mauaji baada ya upande wa ushahidi kutomtia hatiani na hivyo shitaka
kubaki kwa washatakiwa wawili.
Mahakama
ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro imeondoa shitaka hilo kwa Mvungi
baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa dhidi yake kuwa hana hatia.
Shitaka
la mauaji kwa sasa limebaki kwa Mariam Saidi ambaye ni mama mkubwa wa
Nasra Mvungi na Omary Mtonga mume wa Mariam Saidi ambao walikuwa
wakiishi na mtoto Nasra kwa kumfungia katika boksi kwa muda miaka
mitatu.
Mtuhumiwa Omari Mtonga akiwa chini ya
ulinzi baada ya kugoma kutoka kwenye chumba cha mahakama ya hakimu
mkazi wakati akirudishwa katika chumba cha mahabasu mara baada ya
kusikiliza kesi inamkabiri ya mauaji ambapo kesi hiyo sasa itasikilizwa
katika mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam. Picha Juma Mtanda.
Mwendesha
mashtaka wa serikali mkaguzi msaidizi wa polisi Aminatha Mazengo
akisoma shitaka la mauaji mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya hiyo
Irvan Msacky,kwa washitakiwa hao wawili alidai mahakamani hapo kuwa
mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro haina mamlaka ya kusikiliza
kesi ya mauaji.
Mazengo
alidai kuwa kesi hiyo kwa sasa tayari imefunguliwa katika mahakama kuu
wa kanda ya Dar es salaam na kwamba inasubiri vikao vya mahakama kuu ili
iweze kusikilizwa.
Akitoa
maelezo ya kuondolewa kwa Rashidi Mvungi katika kesi hiyo Hakimu mkazi
Irvan Msacky alisema kuwa ameondolewa katika shitaka la mauaji kutokana
na ushahidi kutoteshereza na kutomtia hatiani moja kwa moja na hivyo
kuondolewa katika kesi ya mauaji.
Wakati
kesi hiyo ikiwa imemalizika kusikilizwa,mshtakiwa Omary Mtonga
alianzisha zogo kwa kutaka apatiwe mwendeno wa kesi ya awali kabla ya
kupelekwa ngazi ya mahakama kuu kanda ya Dar es salaamu.
Aidha
kutokana na kuonyesha hali hilo mwendesha mashataka Mazengo alimweleza
Mtonga kuwa hiyo ni haki yake ya msingi kupatiwa mwenendo wa kesi yake
hivyo atapatiwa hati hiyo kabla ya kurudishwa magereza,kuwa ilikuwa
katika hatua ya uchapishaji.
Hata
hivyo Mtonga baada ya kujibiwa hivyo hakuridhika na kuendelea kugoma
kutoka ndani ya mahakama hali iliyomlazimi hakimu mkazi Msacky kuwaamuru
askari kumuondoa kwa nguvu mahakamani hao ili iweze kusikiliza kesi
nyingine.
إرسال تعليق