Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati akiwa pamoja na ujumbe
kutoka Tanzania walipokutana na ujumbe wa shirikala fedha la kimataifa
(hawapo kwenye picha ). Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na kushoto ni Gavana
wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu , akifuatiwa na Gavana msaidizi wa Benki
kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba.

Mkurugenzi
wa Idara ya Afrika wa IMF kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara
Bi. Antoinette Sayeh akiwa na ujumbe kutoka IMF wakizungumza na ujumbe
kutoka Tanzania (hawapo kwenye picha).Katika kikao hicho walizungumzia
zaidi suala la Tanzania kuzidisha nguvu katika kuboresha sera za kukuza
uchumi.

Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akifurahia jambo aliloambiwa na
Bw.Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika
sehemu ya Mashariki wakati wa mkutano uliofanyika kati ya ujumbe kutoka
Tanzania na Shirika la fedha la Kimataifa mjini Washington DC.

Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akitoa maelezo ya jinsi Tanzania
inavyoboresha uchumi wake kwa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa (IMF)kwa
nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara Bi. Antoinette Sayeh wa
katikati. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji
Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na kushoto ni Gavana wa Benki
kuu Prof. Benno Ndulu , akifuatiwa na Gavana msaidizi wa Benki kuu ya
Tanzania Bi. Natu Mwamba.

Bw.
Kamran Khan Makamu wa Rais wa shughuli za operesheni za mfuko wa
Changamoto za Milenia akizungumza katika mkutano wa (MCC/Chamber of
commerce )akisikilizwa kwa makini na wa jumbe kutoka mfuko wa Changamoto
za millennia na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya aliyekaa
mbele.

Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya, akifuatilia kwa makini mkutano huo wa
mfuko wa Changamoto za millenia/Chamber of Commerce Uliokuwa ukifanyika
hapa mjini Washington DC).

Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akizungumza katika mkutano huo wa
Changamoto za Milenia/Chamber of Commerce uliofanyika mjini Washington
DC. Aliyeko nyuma ya Mhe Waziri ni Bw. Laston Msongole ambaye ni
Mtendaji Mkuu wa mfuko wa milenia wa awamu ya pili.
إرسال تعليق