Mhe. Saada Mkuya akutana na Bi.Sayeh pamoja na MCC/Chamber of Commerce


Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati  akiwa pamoja na ujumbe  kutoka Tanzania walipokutana na ujumbe wa shirikala fedha la kimataifa (hawapo kwenye picha ). Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile na kushoto ni Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu , akifuatiwa na Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania  Bi. Natu Mwamba.
DSC_5384
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa IMF kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara Bi. Antoinette Sayeh akiwa na ujumbe kutoka IMF wakizungumza na ujumbe kutoka Tanzania (hawapo kwenye picha).Katika kikao hicho walizungumzia zaidi suala la Tanzania kuzidisha nguvu katika kuboresha sera za kukuza uchumi.
DSC_5385
Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya akifurahia jambo aliloambiwa na Bw.Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki wakati wa mkutano uliofanyika kati ya ujumbe kutoka Tanzania na Shirika la fedha la Kimataifa mjini Washington DC.
DSC_5389
Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya akitoa maelezo ya jinsi Tanzania inavyoboresha uchumi wake kwa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa (IMF)kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara Bi. Antoinette Sayeh  wa katikati. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha  na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius Likwelile na kushoto ni Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu , akifuatiwa na Gavana msaidizi wa Benki kuu ya Tanzania  Bi. Natu Mwamba.
DSC_5478
Bw. Kamran Khan Makamu wa Rais wa shughuli za operesheni  za mfuko wa Changamoto za Milenia akizungumza katika mkutano wa (MCC/Chamber of commerce )akisikilizwa kwa makini na wa jumbe kutoka mfuko wa Changamoto za millennia na Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya aliyekaa  mbele.
DSC_5480
Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya, akifuatilia kwa makini mkutano huo wa mfuko wa Changamoto za millenia/Chamber of Commerce Uliokuwa ukifanyika hapa mjini Washington DC).
DSC_5484
Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya akizungumza katika mkutano huo wa Changamoto za Milenia/Chamber of Commerce uliofanyika mjini Washington DC. Aliyeko nyuma ya Mhe Waziri ni Bw. Laston Msongole ambaye ni Mtendaji Mkuu wa mfuko wa milenia wa awamu ya pili.

Post a Comment

Previous Post Next Post