Dada mmoja aliyedaiwa kuwa mjamzito usiku wa Ijumaa iliyopita
alizua tafrani na kusababisha onesho la Yamoto Band kusimamishwa baada
ya kuvamia jukwaa na kufanya ndivyo sivyo huku kitumbo chake kikiwa
kimejichomoza kiuchokozi kufuatia kuachwa wazi.
Kisa hicho cha kushangaza kilitokea ndani ya Ukumbi wa White House
uliopo Kimara jijini Dar ambapo Yamoto Band kwa kushirikiana na Bendi ya
African Stars ‘Twanga Pepeta’ walikuwa wakifanya makamuzi ya pamoja.
Katika tukio hilo, dada huyo na mwenzake walikuwa wakilivamia jukwaa
na kuwasonga wanamuziki ambapo mabaunsa waliposhindwa kuwadhibiti
waliamua kuzima muziki na kuwasihi wateremke chini wakatii.
إرسال تعليق