DHAMBI?
Neema Pangani, mkazi wa jijini Dar alijikuta akiangua kilio kanisani
wakati mumewe Daniel Mhina alipokuwa anamuoa mke wa pili, Irene Lema,
Risasi Mchanganyiko lina stori kamili.
Neema Pangani, akilia baada ya mumewe kuoa mke wa pili.
Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita katika Kanisa la Evangelistic
Assemblies of God (EAGT) Bonde la Baraka lililopo maeneo ya Alimaua
Kijitonyama jijini Dar, ambapo Mchungaji Kiongozi Asheri Mwaisunga
ndiye aliyebariki ndoa hiyo.
Wakati ndoa inafungwa katika kanisa hilo, mke halali wa Daniel, Neema
ambaye naye ni muumini wa kanisa hilo, aliamua kutoka nje na kuangua
kilio. “Ndoa yangu na Daniel tulifunga Desemba 15, mwaka 1991 katika
Kanisa la Evangelistic Assembies of God Tanzania (EAGT), Uzuri Manzese
jijini Dar ambapo mchungaji Asheri Mwaisunga (huyohuyo aliyefungisha ya
pili) ndiye aliyefungisha ndoa hiyo.
Mume akisaini hati ya ndoa.
“Wakati naposwa na mume wangu Daniel nilikuwa tayari nina mtoto
ambaye nilikuwa nimezaa na mwanaume mwingine lakini nikasikia kuna mama
alikuwa anataka Daniel amuoe ndugu yake, nikamuuliza mume wangu akasema
hapendi kupangiwa mtu wa kumuoa kwa sababu ndoa ni ya watu wawili na
mimi ndiye nilikuwa chaguo lake,” alisema Neema na kuzidi kumwaga
maelezo kuwa, mchungaji huyo aliposikia matatizo yao, alimshauri Daniel
atafute mwanamke mwingine akidai yeye hana kizazi.
Kwa upande wake Daniel, alijitetea kuwa yeye amefunga ndoa ya bomani
Ijumaa iliyopita na pale kanisani alikuwa akibariki na amefanya hivyo
baada ya kugundua mke wake ana matatizo.
Mke akisaini hati ya ndoa.
“Ni kweli nimefunga ndoa lakini ni ya bomani na nilitoa tangazo siku
21 kabla, hakukuwa na kipingamizi chochote na pale kanisani juzi
nilikuwa ninabariki ili nipate baraka kutoka kwa mchungaji wangu ambaye
nilimuomba baada ya kuona kwamba mimi ni muumini mzuri,” alisema na
kusisitiza mkewe huyo wa zamani alikuwa na matatizo.
Cheti cha ndoa ya kwanza.
Mchungaji Asheri Mwaisunga alipotafutwa kwa njia ya simu alijitetea
na kudai kuwa yeye hakufungisha ndoa hiyo ila alikuwa akiibariki baada
ya kufungwa bomani: “Mimi sikufungisha hiyo ndoa kwani tayari
walishafungishwa na Mkuu wa Wilaya na baada ya pale ndiyo wakaja
kanisani kwa ajili ya kubarikiwa, mkitaka vielelezo kamili kuhusu hilo
nendeni kule mtapata.”
Hata hivyo gazeti hili lilinasa picha za Daniel akionekana kusaini
cheti cha ndoa kanisani hapo licha ya mchungaji na Daniel kudai pale
walikwenda kubariki.
إرسال تعليق