STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu na Mtangazaji
Penniel Mwingila ‘Penny’ ambao wote kwa nyakati tofauti wamewahi kuwa na
uhusiano wa kimapenzi na mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
baada ya kuona habari za mwenza wao huyo wa zamani akiwa na mpenziwe
mpya, Zali zinapamba moto kila siku, wameibuka na kudai hawababaishwi
nazo, kwani hivi sasa wameamua kuingia kazini kwa kufanya bonge la
project.
Mtangazaji Penniel Mwingila ‘Penny’.
Akizungumza kwa niaba ya mwenzake, Penny alisema kelele za kila siku
wamezichoka na baada ya kukaa pamoja, wameona hiki ni kipindi cha kupiga
kazi badala ya kupoteza muda.
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
“Tumeamua kuandaa filamu yetu ya pamoja ambayo ninaamini itakuwa ni
kali na ya aina yake. Tumepoteza muda mwingi na hivi sasa tunahitaji
kufanya kazi, tunachowaomba mashabiki wakae tayari kutupokea na hatutaki
tena kushabikia mambo ya Zali na Diamond kwa sababu hayatuhusu,”
alisema.
إرسال تعليق