Mwanamke mmoja, Kudra Janja mkazi wa Kijiji cha Bwai, wilayani
Butiama mkoani Mara amelipuliwa kwa petroli na mumewe, Simon Otieno kwa
kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.Katika tukio hilo pia mtoto
aliyejulikana kwa jina la Tatu Simon (1) alifariki dunia muda mfupi
baada ya kuungua kwa moto katika unyama huo uliofanywa na baba yake
mzazi.
Habari kutoka katika kijiji hicho zinasema kwamba mume wa mama huyo,
Simon aliamua kuwamiminia petroli mke na mtoto wake kupitia dirishani
kisha kulipua kwa moto chumba ambacho wawili hao walikuwa wamelala Machi
31, mwaka huu.
Kudra ameungua vibaya mwili mzima na alilazwa katika Hospitali ya
Mara na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza
wakati mtoto wake alikutwa ndani ya nyumba hiyo akiwa ameungua vibaya
na baadaye kufariki dunia.
Mama mdogo wa Kudra aliyejitambulisha kwa jina la Bahati Magesa
aliliambia gazeti hili kuwa tukio hilo lilitokea nyumbani kwa mjomba wao
saa 10 usiku.“Kisa cha tukio hili ni ugomvi wa siku nyingi unaotokana
na wivu wa mapenzi kwa watu hawa ambao wameishi pamoja kwa muda wa mwaka
mmoja tu,” alisema Bahati.
“Otieno alikuwa akimtuhumu mke wake kwamba alikuwa na uhusiano wa
kimapenzi na watu wengine lakini baadaye ugomvi huo uliisha na wakawa
wanaendelea na maisha yao vizuri.“Baada ya tukio hili Kudra ambaye ni
mtoto wa dada yangu aliniambia kuwa mumewe aliingia ndani akiwa na dumu
la petroli na alipomuuliza la nini alimuambia alale, halimhusu.
“Baadaye alimwaga mafuta dirishani akachukua kibiriti na kutoka nje
akawasha na kuacha mlipuko mkubwa na yeye kutokomea
kusikojulikana.“Baada ya moto kulipuka, Kudra alipiga yowe ndipo mjomba
wake, Obadia Janja alikimbilia na kwenda kumuokoa na akamtoa nje na
mtoto wake wakati moto unawaka kwa kasi.
“Mama alikuwa ameungua mwili mzima na mtoto aliungua vibaya sana na
baada ya muda mfupi aliaga dunia,” alisema Bahati.Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Mara, Philip Kalangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Tumeanza kumtafuta Simon Otieno ambaye amefanya tukio la kinyama na linapaswa kulaaniwa na kila mmoja. Ninaiomba jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi,” alisema Kamanda Kalangi.
“Tumeanza kumtafuta Simon Otieno ambaye amefanya tukio la kinyama na linapaswa kulaaniwa na kila mmoja. Ninaiomba jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi,” alisema Kamanda Kalangi.
إرسال تعليق