MVUA ILIYONYESHA USIKU WA KUAMKIA LEO YASABABISHA MAFURIKO KIWANDA CHA SUKARI CHA TPC .

Eneo la kuegesha gari la zima moto katka kiwanda hicho ikiwa imejaa maji.
Hili si bwawa ni uwanja wa michezo wa Limpopo uliopo katika kiwanda cha sukari cha TPC ,kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha mafuriko katika kiwanda hicho pamojana vijiji vya jirani vinavyozunguka kiwanda hicho.
Hivi ndivyo ilivyokuwa ikionekana katika eneo la kiwanda baada ya mvua zilizonyesha usiku wa jana na kusababisha mafuriko katika kiwanda hicho.
Baadhi ya wafanyakazi katika kiwanda hicho wakitizama mafuriko yalivyo athili maeneo mbalimbali katika kiwanda hicho.
mafuriko katika eneo la kiwanda
Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wakiwa wameketi wasijue nini cha kufanya baada ya maji kuingia katika ofisi zao.
Kituo cha mafuta cha Puma kilichopo ndani ya kiwanda cha TPC kikiwa kimeenea maji.
Eneo la ofisi katika kiwanda hicho.
Hivi ndivyo ilivyoonekana wakati wa asubuhi leo .
Maji yalieneo katika maeneo mengi ya jirani na TPC.
Baadhi ya wafanyakazi katika kiwanda cha sukari cha TPC wakijaribu kuhamisha vitu mbalimbali baada ya nyumba zao kujaa maji,taarifa za awali zinadai zaidi ya watiu 100 wameathirika na mafuriko hayo huku wengine wakipoteza vyakula.hata hivyo tayari serikali mefika eneo la tukio kwa ajili ya kuangalia namna bora ya kusaidia wananchi walioathirika kutokana na mafuriko hayo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Post a Comment

أحدث أقدم