WAZIRI WA UCHUKUZI ARIDHISHWA NA MAENDLEO YA UJENZI WA JENGO JIPYA LA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA (TPA)

 Waziri wa Uchukuzi, Samweli Sitta (wa pili kutoka kulia) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Awadh Massawe, wakati akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Mamlaka hiyo leo mchana. Wa kwanza Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka.
 Mbunifu majenzi  kutoka kampuni ya K &M Acrplans (T) ltd, ambao ndio washauri wa ujenzi wa Jengo hilo, Arch. Albert Mwambafu, akitoa maelezo kwa Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta ya sehemu mbalimbali za jengo hilo, leo mchana wakati Waziri huyo alipotembelea jengo hilo kuona maendeleo ya Ujenzi wake. Jengo hilo litakuwa na ghorofa 35, lakini litakuwa na ofisi mbalimbali na Ukumbi utakaoweza kuchukua watu 1,200 kwa wakati mmoja.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Awadhi Massawe (wa tatu kutoka kushoto), akitoa maelezo ya namna ukumbi ulioko kwenye jengo utakavyokuwa kwa Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, leo mchana wakati Waziri huyo alipotembelea jengo hilo kuona maendeleo ya ujenzi wake.
 Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta akiangalia Boya ya Kupakulia mafuta la SPM, kupitia juu ya jengo jipya la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA),leo mchana wakati alipotembelea jengo hilo kuona maendeleo ya ujenzi wake.Jengo hilo linatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu.
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, akitoa maelekezo kwa viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakandarasi na viongozi kutoka Wizara ya Uchukuzi, baada ya kuangalia maendeleo ya jengo jipya la leo mchana. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

Post a Comment

أحدث أقدم