MWANA HERI KULA MCHICHA KWA FURAHA KULIKO BATA KWA KARAHA!


Niaje…niaje watu wa Mungu? Tupo vizuri…si ndiyo eeh. Basi sawa kozi kona hii ni mzuksi kinomanoma. Ama nene? Basi ni mpango mzima wana. Hapa ni mwendo wa kusanuka na kama vipi ukiona spidi ni kubwa unaruhusiwa kuomba poo. Usijidai kukomaa utapasuka bure. Huu mziki mnene wazazi.
Tudei bana ngoja tupige mastori moo ya masela wa tauni. Najua samu pipo tena makachaa wangu kabisa dizaini kama watanimaindi bati kama mbwai iwe mbwai tu, mkimaindi kimpango wenu makachaa. Sasa mimi si ndo jembe lenu la kuwasanua?
Ebana kuna ishu moko ambayo naona kama inazingua mashori. Eti msela ana mbebiz wake kitu na boksi kabisa na wamesavaivu kwa miaka bee bati anaogopa kumpeleka kwa fasi ya geto.Kuna ishu ambayo masela hawajashtuka. Unanyaka kwamba shori anapoona kaka mkubwa hataki kumpeleka kwa mahomu kwake, anakuwa na mawazo diferenti kuhusu kachaa.
Festi, anajua labda msela ana mai waifu kitu cha famili au anachili na manzi mwingine so hataki shori awe anapajua skani. Ukweli ni kwamba shori anaweza akawa anahisi vitu kibwena ikiwemo kujiona labda si mkare au hana hadhi ya kuoneshwa geto.
Enewei, vyote hivyo vinawezekana bati niamini mimi kuwa mageto ya baadhi ya washkaji hayaingiliki. Chukua hiyo kutoka kwangu. Kama siyo kwamba mageto hayana hadhi basi ujue mazingira si salama so masti ujiweke mbali na watoto wazuri.
Anayebisha kwamba baadhi ya mageto ya wana ni machafu anyooshe kidole! Thubutu yako! Siyo sekreti mazee baadhi ya mageto ya wana ni aibu ileile.Chukua kutoka kwangu kuwa mageto mengi ya washkaji ni machafu hatare kiasi kwamba kama akimpeleka shori haliingiliki! Achilia mbali mazingira machafu na harufu kali, ukizama kwa rumu hicho kitanda chenyewe kipo vululuvuluu.
Mazee si ajabu ukakuta shuka lina wiki mbili halijafuliwa hadi limechenji rangi jamaa yangu.
Kama manzi akitaka kukorofishana na jamaa yake mwenye laifu la dizaini hiyo, ajifanye kukomaa apelekwe geto uone kama hapajachimbika.
Mara utasikia pale geto nachili na mshkaji wangu au madogo ilimradi tu asimpeleke mahomu.
Halafu mazee ukikutana na msela kama huyo kitaani ana mbwembwe hatare. Bonge la sharobaro na tisheti ya wasafi klaski mwendo mdudo kumbe geto hakuingiliki au si ajabu mwana kadandia kwa msela wake.
Majembe yangu mmenisoma? Tusimaindiane wana! Kama vipi kitu cha wikiendi hichooo…nduki!

Post a Comment

Previous Post Next Post