Mshtuko! Weka pembeni mahaba niue waliyokuwa wakioneshana, staa wa
sinema za Kibongo, Shamsa Ford amefunguka rasmi kuhusu kuvunjika kwa
ndoa yake ya kimila aliyofunga na mwanaume wake wa siku nyingi, Dickson
‘Dick’ akikiri kuwa amepoteza muda mwingi kwa mtu ambaye hakuwa na
mapenzi ya dhati kwake.
Alipotafutwa Dick, simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.
CHANZO: IJUMAA WIKIENDA
Shamsa Ford akicheka baada ya kuulizwa swali alipotembelea Global TV Online.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Shamsa alitiririka kwamba mara
nyingi alikuwa akichezea kichapo tena akiwa na ujauzito wa miezi minne
wa mtoto wao, Terry lakini kipindi chote hicho alikuwa akivumilia ili
kukwepa aibu na kumlindia heshima.
Shamsa Ford akiwa na mumewe wake, Dickson Matoke.
“Dick ameninyanyasa kwa muda mrefu lakini kuepuka aibu ya kuwa
mastaa hawatulii, nikawa navumilia kipigo kikali hivyo niliamua kuachana
naye tangu Oktoba, mwaka jana na sikutaka kusema ila sasa nimeweka wazi
kutokana na yeye kuanika mambo yetu kwenye mtandao wa kijamii,” alisema
Shamsa.Alipotafutwa Dick, simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.
CHANZO: IJUMAA WIKIENDA
إرسال تعليق