Baadhi
ya Maaskofu wa Kanisa la Gwajima na maaskofu rafiki wa makanisa ya
Pentekoste wakiongea na Gwajima (Hayupo pichani) ambaye alikuwa akiwapa
maelekezo kabla ya kuondoka kwenda kuhojiwa jeshi la Polisi mchana wa
leo.
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima mapema leo ameibua hofu
kubwa kwa majirani na waumini wake waliokuwa wametanda nje ya nyumba
yake baada ya Jeshi la Polisi kuvamia kwake kwa lengo la kumchukua
kwenda Polisi Central (Makao maalum ya Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es
Salaam).
Askofu Gwajima.
Mbilinge
hilo lililoanza majira ya saa 12, asubuhi kufuatia magari ya Polisi
matatu kufika kwake na kumtaka wamchukue, hata hivyo Askofu Gwajima
hakuwa tayari kufungua mlango wala kutoa ushirikiano hali iliyozua
taharuki kwa majirani.
Kwa
mujibu wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo, walieleza kuwa, baada ya
kuona magari ya Polisi yamepaki nje ya nyumba ya Askofu Gwajima,
walianza kupatwa na wasiwasi hali iliyozua fununu huenda kuna jambo baya
limetokea.
Waumini wa Askofu Gwajima wakiwa wametanda nje huku wakilisindikiza gari lililombeba Askofu Gwajima kutoka nje ya nyumba yake.
Mmoja
wa majirani hao ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake, alibainisha
kuwa, baada ya kuona gari za Polisi zipo nje ya nyumba ya Gwijima
alisogea kwa lengo la kutaka kujua kulikoni ndipo alipobaini kuwa Polisi
hao walikuwa wanamtaka Gwajima ambaye hata hivyo alikuwa ndani pasipo
kufungua geti la nyumba yake.
“Nilisogea
kuhoji kwa jirani yangu lakini nilipoona Polisi ilibidi nirudi. Lakini
baada ya muda waumini wake nao walianza kukusanyika na kukaa nje ya
nyumba yake” alieleza jirani huyo, majira ya saa mbili asubuhi.
Mtumshi
wa Mungu Mtume Dk. Vernon Ferdnandes wa AGAPE, akiwa eneo la tukio
akiwa ameungana na maaskofu wengine waliofika kuungana na mwenzao Askofu
Gwajima.
Hata
hivyo, Moblog iliyokuwa eneo la tukio hilo kuanzia majira ya saa moja
asubuhi, ilianza kushuhudia umati mkubwa wa waumini wa Askofu Gwajima
ukisogea eneo hilo la nyumba yake na kutanda nje ya geti.
Waumini
hao walipofika hawakuwa tayari kuongea na mtu yoyote hapo nje zaidi wao
kwa wao walionekana kuonyeshana ishara maalum huku wakijaribu
kufuatilia mienendo ya Polisi hao ambao walifika na magari zaidi ya
matatu, huku magari hayo matatu ikiwemo Suzuki, Land cruiser namba
T337AK na Pick up aina ya Ford namba PT 288, yaliyoonekana hapo ambapo
walikuwa wakifanya mawasiliano yao.
Picha
iliyopigwa mapema na Modewji blog, kabla ya wafuasi wa Askofu Gwajima
hawajaanza kufika, ambapo gari la Polisi likonekana kuweka doria huku
magari mengine yanayoonekana kwa mbele ya gari hilo ni ya maafisa wa
Polisi waliokuwa wamevalia mavazi ya kawaida.
Kadri
muda ulivyozidi kwenda ndipo waumini wa Askofu Gwajima walikuwa
wakiongezeka kwenye eneo hilo, ambapo majira ya saa sita mchana magari
hayo ya jeshi la Polisi yaliondoka nyumbani kwa Askofu Gwajima moja
moja, huku waumini hao wakiendelea kufuatilia mwenendo wa kila
aliyesogea eneo la nyumba hiyo ambayo pia wandishi wa habari tuliokuwa
hapo nje.
Baadhi
ya waumini walieleza kuwa, wakati wakiwa katika kujiandaa na maombi
pale Kawe wanapokuwa na maombi yao ya kila Ijumaa na Jumamosi ambayo
kabla ya Ibada, walishangaa kutomuona Askofu Gwajima kufika kwenye eneo
hilo la Kawe, ndipo walipopatwa na wasiwasi na walipowasiliana naye,
ndipo walipoamua wote kwa pamoja kutoka Kawe kwenda Sala Sala kwa lengo
la kushuhudia kulikoni na kukuta jeshi hilo la Polisi likiwa limezingira
nyumba hiyo kwa lengo la kumchukua.
Hata
hivyo, vyanzo mbalimbali vya ‘Kiintelijinsia’ vilieleza kuwa, Jeshi
hilo lilipoona umati wa waumini wa Askofu Gwajima kuongezeka kila
wakati, waliamua kuwasiliana na viongozi wao wa juu na ndipo walipoamua
kuondoka.
Wakili
wa Askofu Gwajima, Peter Kibatara akiongea machache kwa wandishi wa
habari dhidi ya Mteja wake, muda mfupi baada ya kutoka nje ya nyumba ya
Gwajima
Wakili wa Gwajima anena.
Hata
hivyo baada ya mashauriano ya muda mrefu, Askofu Gwajima aliweza kutoka
huku akiwa ndani ya gari lenye namba T 159 DDH, akiwa amekaa nyuma na
walinzi wake wa Usalama wawili waliovalia makoti na mawili meusi, ambapo
Wakili Peter Kibatala aliweza kukaa mbele huku akisisitiza kutoonge
lolote kwa mteja wake.
Baada
ya kutoka gari hilo nje ya geti, waumini wake hao walikuwa wakiita
Baba! Baba! Baba!, kwa lengo la kutaka kumuona na kumpa mkono, lakini
ilishindikana huku Wakili wake akisisitiza kuwa mteja wake hatokuwa
tayari kuongea na wandishi wa habari, lakini baada ya kubanwa na
waandishi wa habari, Kibatara aliweza kuongea machache!.
“Tunaelekea
Polisi central makao makuu kuutikia wito wa jeshi la Polisi waliofika
hapa tokea alfajiri. Hivyo baada ya hapo ndipo tutaongea na wandishi wa
habari. Mambo yote ni ya kisheria hivyo baada ya wito kukubali ndipo
tutatoa taarifa hichi ndipo tulichokubaliana” alieleza Wakili Kibatara.
Hata
hivyo baada ya kuongea na waandishi wa habari, gari hilo lilitoka eneo
hilo kwa mwendo kasi huku magari mengine ya maaskofu nao yakiunga kwa
mwendo kasi yakimsindikiza.
Msomaji unaendelea kuperuzi Modewji blog tutaendelea kuwaletea kinachoajili huko Polisi baada ya muda.
Wakili
wa Askofu Gwajima, Peter Kibatara akiondoka eneo la nyumba ya Gwajima
huku Askofu Gwajima akiwa ndani ya gari hilo kwa nyuma.
Baadhi
ya waumini wa Askofu Gwajima wakionekana na majonzi baada ya Askofu
Gwajima kuanza kutoka ndani ya nyumba yake akiwa ndani ya gari (halipo
pichani) ambapo baadhi ya waumini wengine walikuwa wakifuta machozi
huku wakiita Baba! Baba! baba!
Mwandishi
Mwandamizi wa mtandao wa Modewji blog, Andrew Chale akiwa eneo la tukio
nyumbani kwa Askofu Gwajima, eneo la SalaSala, ambaye alipiga kambi
kuanzia asubuhi ya leo hadi majira ya mchana wa saa nane baada ya Askofu
Gwajima, kutii amri ya kukubali wito wa kwenda Polisi Centro… Hivyo
endelea kuperuzi mtandao huu kwa habari zaidi.
Post a Comment