NI SHIDA! Msanii wa filamu Bongo, Michael Sangu ‘Mike’ anadaiwa kuipasua ndoa ya muigizaji mwenzake, Halima Yahya ‘Davina’ na mumewe Abdallah Shakoor baada ya kutuhumiwa kutembea na msichana huyo mwenye watoto watatu.
Chanzo makini kililiambia Risasi Mchanganyiko kuwa kufuatia tuhuma
hizo za muda mrefu, Shakoor anadaiwa kufika ofisini kwa wawili hao
Magomeni jijini Dar es Salaam na kufanya fujo kubwa, zilizosababisha
Davina kuondoka nyumbani kwake na sasa anaishi kwa ndugu zake.
Katika sherehe ya bethidei ya mtoto wao hivi karibuni iliyofanyika katika Hoteli ya Lamada, gazeti hili lilimshuhudia mume huyo akisusa baada ya kugundua kuwa Mike alikuwa ni mmoja wa wasimamizi wa sherehe hiyo.Davina alipotafutwa ili kuzungumzia madai hayo alisema; “Ni kama ulivyoona, ni kweli hakuna maelewano kwenye ndoa yetu, kila ninayefanya naye kazi ananituhumu nina uhusiano naye, Mike ni kiongozi wangu tupo ofisi moja, sasa iliniuma sana alivyoenda kufanya fujo ofisini wakati siyo kweli, namheshimu sana Mike na Thea mkewe ni rafiki yangu siwezi kufanya kitendo kama hicho.”

Kwa upande wake, Mike alikiri kufanyiwa fujo na mume wa Davina
ofisini lakini akadai hana uhusiano na mwanamke huyo bali ni mfanyakazi
mwenzake, anamheshimu na ni rafiki wa mkewe Thea.Salome Urassa ‘Thea’
ambaye ni mke wa Mike, alipoulizwa juu ya sakata hilo, alisema wakati
hayo yakitokea alikuwa Morogoro kikazi na hivyo hawezi kuyazungumzia,
lakini akasisitiza kuwa yeye na Davina ni marafiki.
Post a Comment