NI SHIDA! MIKE SANGU ANADAIWA KUWA KATIKA MAHUSIANO NA DAVINA

NI SHIDA! Msanii wa filamu Bongo, Michael Sangu ‘Mike’ anadaiwa kuipasua ndoa ya muigizaji mwenzake, Halima Yahya ‘Davina’ na mumewe Abdallah Shakoor baada ya kutuhumiwa kutembea na msichana huyo mwenye watoto watatu.

Msanii wa filamu Bongo, Michael Sangu ‘Mike’.
Chanzo makini kililiambia Risasi Mchanganyiko kuwa kufuatia tuhuma hizo za muda mrefu, Shakoor anadaiwa kufika ofisini kwa wawili hao Magomeni jijini Dar es Salaam na kufanya fujo kubwa, zilizosababisha Davina kuondoka nyumbani kwake na sasa anaishi kwa ndugu zake.
Katika sherehe ya bethidei ya mtoto wao hivi karibuni iliyofanyika katika Hoteli ya Lamada, gazeti hili lilimshuhudia mume huyo akisusa baada ya kugundua kuwa Mike alikuwa ni mmoja wa wasimamizi wa sherehe hiyo.Davina alipotafutwa ili kuzungumzia madai hayo alisema; “Ni kama ulivyoona, ni kweli hakuna maelewano kwenye ndoa yetu, kila ninayefanya naye kazi ananituhumu nina uhusiano naye, Mike ni kiongozi wangu tupo ofisi moja, sasa iliniuma sana alivyoenda kufanya fujo ofisini wakati siyo kweli, namheshimu sana Mike na Thea mkewe ni rafiki yangu siwezi kufanya kitendo kama hicho.”
Msanii wa filamu Bongo, Halima Yahya ‘Davina’.
Kwa upande wake, Mike alikiri kufanyiwa fujo na mume wa Davina ofisini lakini akadai hana uhusiano na mwanamke huyo bali ni mfanyakazi mwenzake, anamheshimu na ni rafiki wa mkewe Thea.Salome Urassa ‘Thea’ ambaye ni mke wa Mike, alipoulizwa juu ya sakata hilo, alisema wakati hayo yakitokea alikuwa Morogoro kikazi na hivyo hawezi kuyazungumzia, lakini akasisitiza kuwa yeye na Davina ni marafiki.

Post a Comment

أحدث أقدم