Muigizaji nyota Wastara Juma.
BAADA ya kunusurika kifo katika ajali ya gari,
ambayo mwenyewe amesema ni ya tisa tokea ajitambue, muigizaji nyota
Wastara Juma, amesema anaamini ana jinamizi la ajali linalomuandama,

Wastara, akiwa katika gari lililokuwa likiendeshwa na msanii
mwenzake, Bond Bin Suleiman majira ya saa nne usiku maeneo ya Tabata,
walipata ajali hiyo baada ya gari lisilofahamika, kukatiza kabla mbele
yao na dereva alipofunga breki ghafla, muigizaji huyo ambaye hakuwa
amevaa mkanda wakati huo, alitoka kwenye kiti na kwenda kujigonga kwa
nguvu kwenye ‘dashboard’.
Kitendo hicho cha kujigonga kwa nguvu kilisababisha kujichana sehemu ya juu ya jicho lake la kulia, kitu ambacho kilimpa maumivu makali. Alipokwenda kupata matibabu katika zahanati ya Kilimanjaro, alihudumiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Akizungumzia ajali hiyo, Wastara, mjane wa nyota wa zamani wa filamu, Juma Kilowoko ‘Sajuki’, alisema kwa jinsi zinavyomuandama mara kwa mara tokea alipopata ajali ya kwanza akiwa na umri wa miaka kumi, anaamini ana jinamizi.
“Si bure, kutakuwa na kitu tu kisicho cha kawaida kwangu, lakini naamini Mungu yupo upande wangu, maana ajali hizi zote ni mbaya ambazo ningeweza kabisa kupoteza uhai,” alisema muigizaji huyo.

إرسال تعليق