UGANDA inasema imekamata watu kadhaa kuhusiana na mauaji ya Mwendesha Mashtaka, Joan Kagezi yaliyotokea wiki iliyopita.
Mwendesha mashtaka huyo aliuawa na watu waliokuwa na bunduki
wakitumia pikipiki na polisi kuanza uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo.
Tangu kuuawa kwa mwendesha mashtaka huyo wiki iliyopita polisi
imekuwa katika msako wa wale waliofanya kitendo hicho na hadi sasa
haijaweza kupata nani anayehusika haswa, lakini jana polisi imesema
huenda imepata fununu.
Polisi walizingira nyumba moja katika kiunga cha Jiji la Kampala
sehemu za Kyengera barabara kuu iendayo kusini magharibi mwa nchi.
Mkuu wa Polisi, Generali Kale Kaihura alifika mahali hapo na
kuielezea BBC kuwa walikuwa wanatekeleza msako baada ya kupata fununu
zinazowahusisha wenye nyumba hiyo na matukio ya mauaji.
Watu waliokamatwa wanafikia watano, wanaume wawili na wanawake watatu.
Kutokana na matukio ya kigaidi katika nchi jirani ya Kenya polisi ya Uganda imekuwa chonjo kukabili vitendo hivyo.
Licha mkuu wa polisi kukataa kufafanua wangapi wamekamatwa, lakini
duru za kuaminika zinasema awalikamatwa watu watano, ambapo wawili ni
wanaume na watatu wanawake.
Kukamatwa kwa watu hao kunakuja siku chache baada ya taarifa kueleza
kuwa polisi inamshikilia mwanaume mmoja ambaye alikuwa anapiga picha
bweni moja karibu na Chuo Kikuu cha Makerere mjini Kampala.
Marehemu Joan Kagezi, mwendesha mashtaka aliyepigwa risasi wiki
iliopita alizikwa mwishoni mwa juma nyumbani kwake. Bado haijabainika
nia ya waliompiga risasi ilikuwa nini.
Marehemu alikuwa anaongoza kesi dhidi ya washukiwa 13 ambao
wanashtumiwa kuhusika na utegaji mabomu yaliowaua watu zaidi ya 70 mjini
Kampala mwaka 2010 katika ukumbi wa kutizama kandanda.
BBC
إرسال تعليق