WAPINZANI
wa Serikali nchini Burundi, wameitisha maandamano makubwa leo ya
kupinga hatua ya Chama Tawala cha CNDD-FDD kumtangaza Rais Pierre
Nkurunziza, wa nchi hiyo kuwania mhula wa tatu katika uchaguzi ujao
(Katiba ya Nchi hiyo hairuhusu mihula mitatu).
Mkuu
wa Chama cha FNL kilichipigwa marufuku nchini humo, Agathon Rwasa,
amepinga vikali uamuzi huo na kusema kwamba unaenda kinyume na Katiba ya
Burundi.
Rwasa,
amesisitiza kuwa, kuteuliwa kwa Rais Nkurunzinza kw aajili yam hula wa
tatu utaitumbukiza nchi hiyo katika matatizo makubwa. Rwasa ndiye
aliyekuwa mpinzani mkuu wa rais Pierre Nkurunziza katika uchaguzi mkuu
wa mwezi Juni, 2010.
Kufuatia
hatua hiyo, wapinzani hao wa serikali kwa nyakati tofauti, wameitisha
maandamano makubwa leo Aprili 26, 2015 kupinga hatua hiyo ya chama
tawala.
Akimtangaza
rasmi Rais Nkurunzinza, Mwenyekiti wa Chama Tawala nchini humo, Pascal
Nyebenda, aliwataka wapinzani wa serikali kuwa watulivu na kuachana na
Rais Nkurunzinza katika masanduku ya kumipigia kura.
Mzozo
wa kisiasa unaendelea kutokota nchini humo ambapo taarifa zinaeleza
kuwa hivi sasa kumezuka ghasia katika mji wa Bujumbura nchini humo kati
ya maafisa wa Polisi na waandamanaji wanaoishtumu serikali kwa kufanya
mapinduzi ya kikatiba.
Waandamanaji
walirusha mawe na kuchoma matairi huku maafisa wa Polisi wakilazimika
kurusha mabomu ya machozi na risasi bandia hewani ambapo ghasia hizo
zinafuatia tangazo lililotolewa siku ya Jumamosi kwamba Rais wa
Nkurunziza ameteuliwa na chama chake kuwania muhula wa tatu wa
urais.Serikali imesema kuwa maandamano hayo si halali.
Kumbukumbu
zinaonyesha kwamba maelfu ya raia wa Burundi wamelitoroka taifa hilo
katika majuma ya hivi karibuni wakihofia kuongezeka kwa ghasia hizo,
huku taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi mnamo mwezi Juni, 2015.
Wakati
hayo yakitokea, mrengo wa upinzani nchini humo unaoundwa na vyama 9,
Aprili 21, 2015 ulimtangaza Jean de Dieu Mutabazi, kuwa ndiye
atayapeperusha bendera yao katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo.
Muungano huo unaojulikana kwa jina la Participatory Opposition Coalition in Burundi (COPA), umemteua Mutabazi kuwa mgombea wake katika uchaguzi huo utakaofanyika Juni mwaka huu.
Muungano huo unaojulikana kwa jina la Participatory Opposition Coalition in Burundi (COPA), umemteua Mutabazi kuwa mgombea wake katika uchaguzi huo utakaofanyika Juni mwaka huu.
إرسال تعليق