Rehema Chalamila aka Ray C amewatoa hofu mashabiki wa muziki wake,
kuwa unene wake haujakiathiri kiuno chake bila mfupa bali kimemwongezea
uwezo wa kukatika kuliko zamani!
Ray C ambaye alitamba na nyimbo kama ‘Sikuhitaji’ na ‘Umeniacha’,
ameiambia Global TV kuwa anahisi uwezo wake wa kukatika umeongezeka
zadii kutokana na unene.
“Sina tofauti na Ray C wa zamani,” alisema. Ray C ni yule yule, kiuno
cha zamani ni kile kile. Sema sasa hivi kina nyama kidogo kwahiyo sasa
hivi nikifanya kidogo tu yaani ni rahisi zaidi kwangu.”
إرسال تعليق