Waziri
wa Uchukuzi, Samweli Sitta (wa pili kutoka kulia) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Awadh Massawe, wakati
akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la Mamlaka hiyo leo
mchana. Wa kwanza Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban
Mwinjaka.
Mbunifu
majenzi kutoka kampuni ya K &M
Acrplans (T) ltd, ambao ndio washauri wa ujenzi wa Jengo hilo, Arch. Albert
Mwambafu, akitoa maelezo kwa Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta ya sehemu
mbalimbali za jengo hilo, leo mchana wakati Waziri huyo alipotembelea jengo
hilo kuona maendeleo ya Ujenzi wake. Jengo hilo litakuwa na ghorofa 35, lakini
litakuwa na ofisi mbalimbali na Ukumbi utakaoweza kuchukua watu 1,200 kwa
wakati mmoja.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Awadhi
Massawe (wa tatu kutoka kushoto), akitoa maelezo ya namna ukumbi ulioko kwenye
jengo utakavyokuwa kwa Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, leo mchana wakati
Waziri huyo alipotembelea jengo hilo kuona maendeleo ya ujenzi wake.
Waziri
wa Uchukuzi, Samuel Sitta akiangalia Boya ya Kupakulia mafuta la SPM, kupitia
juu ya jengo jipya la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA),leo mchana
wakati alipotembelea jengo hilo kuona maendeleo ya ujenzi wake.Jengo hilo
linatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu.
Waziri
wa Uchukuzi, Samuel Sitta, akitoa maelekezo kwa viongozi wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakandarasi na viongozi kutoka Wizara ya
Uchukuzi, baada ya kuangalia maendeleo ya jengo jipya la leo mchana. (Picha na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
Post a Comment