YANGA BINGWA


 Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kumalizika kwa mchezona Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.
 Amis Tambwe akipokea mpira kutoka kwa Mwamuzi Zacharia Jacob kutoka Kisarawe mkoani Pwani, baada ya kufunga"Hat Trick" na kufanya kurejea record yake ya msimu uliopita akiwa na Simba ya kufunga hatitrick  2. na leo kufikisha idadi ya magoli 14 na kushika nafasi ya pili ya ufungaji
 Mashabiki wakishangilia.Picha:Francis Dande
YANGA RAHAAAAA!! Timu ya Yanga leo imejinyakulia pointi 3 na magoli 4 muhimu kutoka mikononi mwa maafande wa Polisi Morogoro na kujidhihirisha kuwa wao ndio mabingwa wa soka la Tanzania kwa msimu huu wa 2014/2015

Matokeo ya leo yameifanya Yanga kufikisha pointi 55 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yeyote ikiwepo Azam na Simba ambazo zinawania nafasi ya pili.

Magoli ya Yanga leo yamefungwa na Hamisi Tambwe (3) na Msuva  na kufanya wachezaji hao kufikisha magoli 17 kwa Simon Msuva na Hamisi tambwe kushika nafasi ya pili kwa ufungaji katika ligi hiyo kwa magoli 14. 
Yanga imebakisha michezo miwili dhidi ya Azam na Ndanda FC ambayo hata ikipoteza haita igharimu zauidi ya kulinda heshima yake.

Post a Comment

أحدث أقدم