Zanzibar. Mawaziri wawili wa Serikali ya Umoja
wa Kitaifa kutoka CUF na wabunge wengine wakongwe wa chama hicho
wamepigwa mwereka kwenye kura za maoni za kutafuta wagombea wa nafasi za
uwakilishi na ubunge kwa majimbo 50 ya Zanzibar.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa uchaguzi wa CUF, Omary Ali Shehe alisema matokeo hayo ni ya awali.
Walioangushwa ni waziri asiyekuwa na Wizara
Maalumu, Haji Faki Shaali ambaye ameangushwa katika Jimbo la Mkanyageni,
sambamba na mbunge wa jimbo hilo, Mohamed Habib Mnyaa na Naibu Waziri
wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati, Haji Mwadini Makame katika nafasi ya
uwakilishi katika jimbo la Nungwi.
Kwa mujibu wa matokeo ya awali, kura hizo
zimewatupa waandishi wa habari waliokuwa wamejitokeza kuwania nafasi
mbalimbali akiwamo mtangazaji mkongwe wa BBC, Ally Saleh ‘Alberto’
ambaye ameangushwa na mbunge wa sasa wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ibrahim
Mohamed Sanya.
Wengine ni Talib Ussi Hamad wa Mwananchi aliyepata
kura 31 katika nafasi ya ubunge Jimbo la Magogoni na kutanguliwa na
Juma Kombo Hamad aliyepata kura 106 huku mbunge anayemaliza muda wake
Kombo Khamis Kombo akiambulia kura 61.
Mwandishi wa Majira, Mwajuma Juma alishika nafasi
ya pili, baada ya kupata kura 11 akiwania nafasi ya uwakilishi jimbo la
Amani, ambapo Khamis Rashid Abeid aliibuka kidedea kwa kura 22, huku
mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Maua Mohamed Mussa akishika mkia
katika nafasi aliyokuwa akiwania ya ubunge wa viti maalumu, Wilaya ya
Mjini.
Mtangazaji wa zamani wa Sauti ya Tanzania Zanzibar
(STZ), Najma Khalfan Juma alipata pigo mara mbili baada ya kuanguka
katika kura za maoni nafasi ya uwakilishi jimbo la Ziwani na nafasi ya
ubunge viti maalumu kupitia Wilaya ya Chakechake, Pemba.
Kwa upande wa uwakilishi wa viti maalumu Wilaya ya
Mjini, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma
Abdulhabib Ferej amepenya kwenye tundu la sindano kwa ushindi wa kura
moja, baada ya kupata kura 91, akifuatiwa na Nunuu Salim Rashid
aliyepata kura 90 na mtoto wa mbunge wa Mji Mkongwe, Rahma Ibrahim Sanya
aliyepata kura 30 huku kura nne zikiharibika.
Mbunge wa Mtambile, Mohamed Abdallah Salim naye
ameanguka katika kura za maoni sambamba na mwakilishi anayemaliza muda
wake, Mohamed Haji Khalid huku Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar
(Suza), Dk Alley Soud Nassor akijitoa kabla ya uchaguzi na nafasi hiyo
ya uwakilishi kunyakuliwa na Abdallah Bakar Hassan.
Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi wa CUF kutoka
Jimbo la Chonga, Abdallah Juma Abdallah ameanguka katika kura hizo
pamoja na mbunge wa jimbo hilo, Haroub Mohamed Khamis huku Mwenyekiti wa
Kamati ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC), Omar Ali Shehe
akishinda kwa kura tisa baada ya kumwangusha Mhasibu wa Kampuni ya simu
ya Zantel, Ali Bakari aliyepata kura 97.
Kwa upande wa ubunge Jimbo la Chakechake, Yusuph
Kaiza Makame ameibuka kidedea kwa kura 84 baada ya kumuangusha Fatma
Omar Juma aliyepata kura 83, huku Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Juma
Duni Haji akishinda kwa kupigiwa kura za ndiyo baada ya mpinzani wake
Ali Juma Khamis kujitoa dakika za mwisho na kupata kura 60 kati ya 61
katika nafasi ya uwakilishi jimbo la Bububu.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Nassor
Ahmed Mazrui amepita katika kura za maoni nafasi ya uwakilishi jimbo la
Mtoni, lakini mbunge, Faki Haji Makame ameanguka
إرسال تعليق