KWELI
mchepuko siyo dili! Kauli hii imedhihirika kufuatia mwanadada, Ashura
Maulid, mkazi wa Ilala jijini Dar, kukumbwa na mauti kwa madai ya
kunyongwa ndani ya gesti na mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la
Charles ambaye inasemekana ni mpenzi waliyekutana kwenye mtandao wa
kijamaii wa Facebook.
Marehemu Ashura Maulid enzi za uhai wake.
Tukio hilo lililojaa majonzi tele na kuacha maswali mengi, hasa kwa
mume wa marehemu, Suleiman Othman, lilijiri Mei 19, mwaka huu kwenye
nyumba ya kulala wageni (jina lipo) iliyopo kandokando ya barabara ya
kutoka Sinza Afrikasana kwenda Kijitonyama kupitia Kituo cha Polisi cha
‘Mabatini’, Dar.
Chanzo kinadai kuwa, enzi za uhai wake, mwanadada huyo alikuwa
akijihusisha na biashara ya kuuza duka la friji maeneo ya Sinza ya
Afrikasana na inasemekana amekuwa ndani ya ndoa na mumewe, Suleiman kwa
miaka 15 na kujaliwa kupata watoto wawili, wa mwisho akiwa na umri wa
mwaka mmoja na nusu.
Akizungumza na Uwazi, Ijumaa iliyopita huku akiwa katika majonzi
mazito, mume huyo alisema Jumanne ya Mei 19, mwaka huu, mkewe alimuaga
anakwenda kazini huku akiumwa, alimtaka apumzike lakini mwanamke huyo
akasema anajiona amepona hivyo ana uwezo wa kumudu majukumu yake.
“Ilipofika saa moja usiku akanitaarifu kuwa ameshatoka kazini. Cha
ajabu mpaka saa nne usiku alikuwa hajafika nyumbani na nilipompigia simu
hakupokea.“Mara kwa mara mke wangu alipokuwa akimaliza kazi na kuanza
safari ya kurudi nyumbani alikuwa ananitaarifu, nachati naye kila wakati
mpaka anafika. Siku hiyo nilikuwa nina majukumu mengi aliponitaarifu
kamaliza kazi ndo’ anarudi sikuwa na presha.
“Sasa ilipofika saa nne mimi nikiwa nyumbani na simu hapokei,
nikashangaa. Mbaya zaidi, baadaye simu yake ikawa haipatikani
kabisa.“Nilifanya jitihada za kumtafuta kwa ndugu na jamaa, vituo vya
polisi na hospitali mbalimbali, ikiwemo Muhimbili kuulizia kwenye wodi
za wagonjwa lakini sikumkuta.
Mume wa marehemu Ashura Maulid.
“Juzi (Mei 20), nilishtuka kupigiwa simu na polisi wa Kijitonyama,
wakaniambia kuna maiti imekutwa mahali (walimficha kama ilikuwa gesti)
na aliyehusika na mauaji ni mwanaume ambaye walianza kufahamiana na mke
wangu kupitia Facebook. Walisema marehemu alionekana alikufa kwa
kunyongwa.
“Waliniambia huyo mwanaume alikimbia baada ya kufanya mauaji hayo.
Palepale ndo’ wakaanza jitihada za kumtafuta mpaka wakamkamata,” alisema
mume huyo.Akiendelea kuelezea tukio hilo alisema kisa cha kugundua kuwa
Charles alikutana na mke wake kwenye Facebook ni siku ya tukio baada ya
mawasiliano waliyoyafanya kwa kipindi kirefu bila yeye kujua.
Alisema ilionesha kuwa, siku hiyo waliamua kuonana laivu ambapo
alimkaribisha dukani kwake na kuondoka naye baada ya kumaliza kazi na
kufunga duka huku akiwa amemtaarifu bosi wake (si mumewe) fedha
zilizopatikana siku hiyo.
“Niliambiwa na rafiki wa mke wangu kuwa siku hiyo mwanaume huyo alifika dukani kwa mke wangu akawatambulisha mashosti zake kuwa ni rafiki yake waliyejuana Facebook. Wakiwa hapo, mke wangu alimpigia simu bosi wake kumwambia siku hiyo aliingiza shilingi milioni moja na laki saba. Huenda hicho ndo’ kilimfanya jamaa amgeuke na kumuua kwa tamaa ya zile fedha,” aliongeza.
“Niliambiwa na rafiki wa mke wangu kuwa siku hiyo mwanaume huyo alifika dukani kwa mke wangu akawatambulisha mashosti zake kuwa ni rafiki yake waliyejuana Facebook. Wakiwa hapo, mke wangu alimpigia simu bosi wake kumwambia siku hiyo aliingiza shilingi milioni moja na laki saba. Huenda hicho ndo’ kilimfanya jamaa amgeuke na kumuua kwa tamaa ya zile fedha,” aliongeza.
Mumewe huyo alisema, haamini kama mkewe alishindwa kuiheshimu ndoa
yake na kuwapa nafasi wanaume wengine tena kwa kwa mtu ambaye
hakufahamiana naye ila kwa kukutana naye kwenye mtandao na kuanzisha
uhusiano kwani yeye alimtosheleza kwa kila jambo.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillus
Wambura alipotafutwa ili aulizwe kuhusiana na tukio hilo, simu yake
iliita bila kupokelewa.Uwazi lilipofika kwenye gesti hiyo ambayo
marehemu alifia chumba Namba 4 lakini wahusika waligoma kutoa
ushirikiano na kudai hakukuwa na tukio hilo.
Kesi hiyo ipo katika Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ faili
Namba KJN/RB/5081/15 TAARIFA YA KIFO huku mtuhumiwa akishikiliwa hapo
baada ya kukamatwa akiwa na gari aina ya Toyota Carina (namba za usajili
zipo).
إرسال تعليق