STAA wa filamu Bongo, Irene Paul ‘Smart Girl’ amezua
 mshangao baada ya kupiga mayowe huku akirusha mikono kushangilia tuzo 
aliyopata jambo lililozua miguno kwa waliomshuhudia.
 
Staa wa filamu Bongo, Irene Paul ‘Smart Girl’ akitahayari wakati wa kuchukua tuzo.
‘Katukio’ hako ‘amazing’ kalishuhudiwa na paparazi wetu mwishoni mwa 
wiki iliyopita ndani ya Jengo la Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar 
kulikokuwa na sherehe ya utoaji Tuzo za TAFA na kuwafanya baadhi ya watu
 kuacha kila kitu kwa muda na kumtumbulia macho.
Msanii huyo alipata tuzo hiyo kwa kipengele cha The Best Actress 
(Supporting Role) kupitia Filamu ya Never Give Up aliyoshirikiana na 
msanii kutoka Nigeria,  Joseph Van Vicker na kuonekana kuchanganyikiwa 
namna hiyo.
Baada ya kuchukua tuzo hiyo, ‘kiruka njia’ wetu alimfuata na 
kumuuliza kulikoni aonekane kupagawa kwa kiwango hicho ambapo alisema 
kutokana na ugumu wa kipengele hicho kwani alikuwa akichuana na watu 
anaowaheshimu sana katika tasnia ya filamu, alioamini wana kiwango cha 
juu kuliko yeye hivyo hakuamini kilichokuwa kinatokea kwa wakati huo.
Post a Comment