Uongozi wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo umekutana na
Uongozi wa klabu ya
Simba SC ukiwakilishwa na Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji
Collin Frisch na mchezaji
Ramadhani Yahya Singano akiandamana na Uongozi wa
Chama cha Wacheaji wa
Mpira wa Miguu (SPUTANZA). Kikao hiki kiliitishwa na
TFF kujadili utata wa
kimtakabta kati ya mchezaji na klabu ya Simba.
Katika kikao cha leo
pande zote zimeeleza kutambua utata ulio ndani ya
mikataba iliyokuwepo
ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa sasa wa
Simba SC.
Kwa pamoja pande hizo
mbili zimekubaliana kuanza mazungumzo ya makubaliano
mapya na hatimaye mkataba
mpya utakaoanza katika msimu mpya wa 2015/16.
TFF imevitaka vilabu
kushirikiana na SPUTANZA na Bodi ya Ligi katika kuweka
mifumo mizuri ya uingiaji
mikataba. TFF inao mkataba mama
(*template*)
ambao vilabu vyote na
wachezaji wanatakiwa waufuate wakati wanaandaa
mikataba yao (*individual
contracts between players and clubs*).
Aidha TFF
imewataka wachezaji kuelewa mikataba kabla ya kutia
sahihi.
TFF itazidi kuboresha
mfumo wa usajili wa wachezaji na mikataba ili kuweka
mazingira sawia kati ya
pande zote mbili (Wachezaji na vilabu)
Makubaliano yamefanyika
leo tarehe 9 Juni 2015 na kusainiwa na:-
- Collin Frisch - Simba SC
- Ramadhan Singano - Mchezaji
- Mussa M. Kissoky - SPUTANZA
- Mwesigwa J. Selestine - Katibu Mkuu - TFF
*IMETOLEWA NA SHIRIKISHO
LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)*

إرسال تعليق