Kwa kocha huyu mtalala na viatu

MSIMU uliopita Ligi Kuu Bara ilipoanza, Simba ilionekana dhaifu na yenye tatizo kwa wachezaji wake kukatikiwa pumzi kiasi cha kuwapa nafasi wapinzani wao ya kuwatawala katika michezo yao.
Karibu kila mchezo waliocheza walitangulia kufunga bao au mabao lakini mwishowe yalirejeshwa na kufanya timu kuwa na wakati mgumu mpaka ligi ilipoenda mapumzikoni mwishoni mwa mwaka.
Baadaye Simba iliamua kuachana na Mzambia Patrick Phiri na kumpa nafasi Mserbia, Goran Kopunovic ambaye, licha ya kujitahidi kuibadilisha timu, tatizo la ukosefu wa stamina liliendelea.
Pengine kwa kulitambua jambo hilo ndiyo maana uongozi wa klabu hiyo chini ya Rais Evance Aveva umeamua kufanya jambo la maana ambalo huenda likawapa wakati mgumu wapinzani wao katika Ligi Kuu msimu ijayo. Hii ni baada ya kuamua kumleta kocha mkali wa mazoezi ya utimamu wa mwili (fikizi), Dylan Kerr kutoka Uingereza.
Mbali na umahiri wake wa kuwaweka wachezaji katika utimamu wa mwili (fitness), lakini ni mahiri wa kufundisha soka la pasi, jambo ambalo Aveva alitamka wazi kuwa ni kocha waliyekuwa wakimsaka kwa muda mrefu kuirejeshea Simba heshima yake.
Aveva alisema Kerr ambaye ataingia mkataba wa mwaka mmoja wenye makubaliano ya kuongezewa mwingine endapo atafanya vizuri licha ya kwamba hana uzoefu katika nchi za Afrika Mashariki, ila wanaamini ataibadilisha timu yao kufuatia kuwahi kufanya kazi Afrika Kusini.
Beki huyo wa zamani wa klabu za Sheffield Wednesday, Leeds United, Reading na Blackpool zilizowahi kutamba kwenye Ligi Kuu ya England anatua Msimbazi akitokea Vietnam.
Mchakato
Aveva alianika mchakato wa kumsaka kocha huyo kuwa ulifanywa kwa umakini mkubwa kabla ya kuafikiana na hatimaye kulazimika kumuanika hadharani ili kukata kiu ya wanachama na mashabiki wa Simba waliokuwa wakichanganywa na taarifa mbalimbali za ujio wa kocha wao mpya.
“Mchakato ulihusisha makocha zaidi ya watano akiwamo Kim Poulsen aliyewahi kuwa Kocha wa Taifa Stars, lakini tuliachana naye baada ya kuingiliwa na mambo fulani hasa kwa wakala wake, na mwishoni turufu ilimuangukia Kerr,” alisema Aveva.
“Tunaamini kwamba Kerr ataisaidia timu yetu kupata mabadiliko makubwa kuweza kuipa mataji mbalimbali Simba, kazi yetu kama uongozi ni kumuandalia mazingira mazuri ya kufanya kazi akiwa na wasaidizi wake.
Usajili

No comments:

Post a Comment