
SIRI
ya kutoswa kwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi kwenye kikosi cha
timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’, kitakachopambana na Gambia kwenye
mechi ya kimataifa ya kirafiki pamoja na Botswana kuwania kufuzu fainali
za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017), zimevuja.
Okwi ametemwa kwenye
kikosi hicho sambamba na mastaa wengine kama Tonny Mawejje, Andrew
Mwesigwa, Moses Oloya, Geofrey Baba Kizito, Daniel Sserunkuma na Derrick
Tekkwo kutokana na sababu mbalimbali.
Habari
za uhakika kutoka Uganda zilisema Okwi ameachwa The Cranes kutokana na
kitendo chake cha kushinikiza wachezaji wa timu hiyo wanaocheza soka la
kulipwa walipwe kiasi kikubwa cha fedha tofauti na wale wanaokipiga
nchini kwao.
إرسال تعليق