Na Woinde Shizza, libeneke la kaskazini blog
Mwendesha magari Randeep Shingh
kutoka jijini Dar es Salam ameibuka mshindi katika mashindano ya kila
mwaka ya mbio za nyika za magari nane-nane rally yaliyotimua vumbi
katika mji wa Arusha mwishoni mwa wiki.
Mashindano hayo yamefanykia kwa
siku mbili mfululizo huku yakishuhudiwa ushindani mkali kwa madereva
hao waliotoka mikoa mbalimbali na Randeep Shingh akiwa na msoma ramani
Guvinder Singh wa gari ya Mitsubishi lancer akiibuka mshindi wa jumla
katika mashindano hayo.
Katika mashindano hayo
yaliyokuwa yakitofauti mwaka huu, baada ya kufungiwa mitambo ya kisasa
ya kidigitali kwa kila gari ili kuwezesha ufuatiliwaji wa kila gari na
njia zitakazopitia kwa ajili ya kuhakikisha kuwa hakuna zengwe wala
suala la madereva kuiba njia na hata kupotea porini.
Zaidi ya madereva 20 kutoka
ndani na nje ya nchi walioshindana zaidi ya Km 198 huku mshindi wa
pili akiwa ni Raj Pal Dhani na msoma raman Sinder Sudle wakiwana na
ghari la Subaru Impreza nafasi ya tatu ikiwa imeshikwa na Gurjit Singh
huku dereva mkongwe wa nchini Tanzania, Gerald Miller akiambulia
nafasi ya sita, HUKU baadhi ya madereva walioshiriki katika mashindano
hayo wakisema yalikuwa magumu mwaka huu huku wengine wakizungumzia
changamoto ya barabara, baadhi ya mashabiki wa mchezo waliojitokeza kwa
wingi kutazama mashindano ya hayo ya Utrack nanenane rally walisema
wamefurahi na kuiomba serikali kuwezesha mashindano haya kufanyika mara
kwa mara
إرسال تعليق