Kutoka Zimbabwe mpaka Simba Sports Club huyu ni kiungo mpya


Klabu ya soka ya Simba imeendelea kujizatiti kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara kwa kusajili wachezaji tofauti tofauti na sasa imemleta Justice Majabvi kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Vicem Hai Phong F.C ya Vietnam amewasili  alfajiri ya August 1 katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
2aaf9db72088f539e4e5920a6dbf5081_412x367
Majabvi ametua Dar es Salaam kwa ajili ya kujiunga na Simba Sports na amepanda boti moja kwa moja kuelekea visiwani Zanzibar kujiunga na timu hiyo ambayo imeweka kambi visiwani humo kabla ya kurejea Dar es Salaam August 6.
fus_bl_salzburg_moniz_nach_body_g.2062877
Hata hivyo taarifa zinaripoti kuwa Majabvi atakuwa na muda wa siku tatu wa kufanya mazoezi na timu kabla ya kusaini mkataba  ili kocha wa Simba Dylan Kerr amuangalie uwezo wake.
news_bmajabvi-250
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 amewahi kuichezea timu ya Dynamos na kufikia hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2008, kwa mara ya kwanza alicheza timu ya taifa ya Zimbabwe July 15 2004 dhidi ya timu ya taifa ya Zambia.
Justice-Majabvi-100413-Inaction-R-300
CHANZO CHA STORY HII>>>BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE

Post a Comment

Previous Post Next Post