Man U Yatambulisha Rasmi Jezi Zake Mpya


jezi4Klabu ya Manchester United imekuwa miongoni mwa klabu ambazo zimetambulisha jei zao leo zitakazotumiwa kwa ajili ya msimu ujao. Klabu hiyo imevunja rekodi kwa kuwa ni klabu inayoingiza kipato kikubwa cha pesa duniani kutokana na utengezaji wa jezi .
jeziBaada ya miaka 13 ya matumizi ya jezi za Nike, Manchester United sasa imeamua kuzindua jezi mpya zitakazotumika katika msimu wa 2015/2016. Man United watatumia jezi zitakazokuwa zinatengenezwa na Kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas ya nchini Ujerumani.
jezi1Man United wamesaini mkataba  wa miaka 10 na kampuni ya hiyo ya Adidas, mkataba wenye thamani ya pound milioni 750 na sasa wataanza kutumia jezi za kampuni hiyo.
jezi2Wakongwe hao (Adidas) wa kutengeneza vifaa vya michezo wanaamini wanaweza kutengeneza kiasi cha pauni bilioni 1.5 kutokana na mauzo ya jezi za Man U kwa muda wa miaka 10 ijayo.
jezi3Mkataba huo kati ya Manchester United na Adidas ni mkataba mnono zaidi kwa klabu hiyo ukilinganisha mikataba ya klabu nyingine ambazo zinatengenezewa jezi na kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na klabu Bayern Munich (pauni milioni 645) na Chelsea (pauni milioni 300).
man u 12
Jezi hizo mpya zitakuwa na muonekano kama ule wa zamani enzi za Ryan Giggs zikiwa na shingo ya V yenye rangi nyeupe na michirizi mitatu kwenye mikono yake. man u 22



man u
man u1
man u21
man u223

Post a Comment

Previous Post Next Post