MAGUFULI ALIVYOPOKELEWA NDANI YA WILAYA YA NJOMBE MKOANI NJOMBE.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Ludewa mjini kabla ya kuanza kuwahutubia ,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo na kuhudhriwa na maelfu ya watu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Ludewa waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Ludewa,aliyepita bila kupingwa Mh Deo Filikunjombe ,akisoma ilani ya CCM aliyokabidhiwa na Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,wakati alipokuwa akihutubia wananchi wa kijiji cha Mlangali wilayani Ludewa
Wananchi wa mji wa Ludewa wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa mpira mjini Ludewa wakimshangilia mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukiwa umezuiwa na Wananchi wa kijiji cha Mavanga wilayani Ludewa huku wakishangilia na kuimba  "JEMBE LA KAZI LIMEINGIA",ambapo Magufuli akiwa ameambatana na Mbunge wa jimbo hilo la Ludewa,Mh Deo Filikunjombe walisimama na kuzungumza na wananchi hao ikiwemo pia kuwaomba kura za kutosha ili wapate ridhaa ya kuwaongoza Watanzania katika awamu ya tano.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya walemavu waliokuwa wamefika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni kumsikiliza sera zake,Dkt Magufulia alieleza kuwa katika Ilani ya CCM,kwa awamu ya tano itawajali walemavu na kuwapa vipau mbele hasa katika masuala ya elimu,ya kijamii pamoja na kuwawezesha kiuchumi ili waweze kujishulisha vyema katika maisha yao ya kila siku
Wananchi wa jimbo jipya la Madaba wakimsikiliza kwa makini mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jukwaani  kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Wananchi wa Mlangali wilayani Ludewa wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hdahara wa kampeni,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia.
Mmoja wa wakazi wa mji wa Ludewa akiwa na bendera yake,huku akimisikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano kwa nafasi ya Urais.
Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukiwasili wilayani Ludewa kutoka mkoani Njombe.
Ngoma ya asili kutoka Ludewa ilipokuwa ikitumbuiza uwanjani hapo
Wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa hadhara wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Ludewa mjini kabla ya kuanza kuwahutubia ,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo na kuhudhriwa na maelfu ya watu.
Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM wakielekea kwenye uwanja wa mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Madaba.
Wananchi wa jimbo jipya la Madaba wakishangilia ujio wa mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli.alipokuwa akipanda jukwaani kuwahutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
Gari ya Mgombea Ubunge wa jimbo la Ludewa,Mh Deo Filikunjombe katika ubora wake
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwa amezuiwa na Wananchi wa kijiji cha Mavanga wilayani Ludewa,ambapo Magufuli akiwa ameambatana na Mbunge wa jimbo hilo la Ludewa,Mh Deo Filikunjombe (hayupo pichani),waliwaomba wananchi hao ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano
Wanamsikiliza Mgombea Urais Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipita kuelekea wilayani Ludewa kuwahutubia wananchi
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Lugalawa wakiwa wamefunga njia wakitaka kumuona mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli na pia kumtaka awasalimie na kuwasikiliza kero walizonazo ili akipata ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika awamu ijayo ya miaka mitano awasaidie
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Lugalawa wilayani Ludewa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,aliposimama kuwasalimia na kuwaeleza kuwa anaomba kura zao za kutosha katika kumuwezesha kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Ludewa Mh Deo Filikunjombe akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mlangali wiliayani Ludewa.
Wananchi wa kijiji cha MLangali wakishangilia jambo
Picha Na Michuzi

Post a Comment

Previous Post Next Post