Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro
chini ya Kocha wake Mkuu Charles Boniface Mkwasa imefanya mazoezi yake
ya mwisho leo asubuhi katika viwanja vya hoteli ya Green Park Kartepe –
Kocaeli nchini Uturuki.
Taifa
Stars ambayo imeweka kambi nchini Uturuki kwa takribani wiki moja,
inajiwinda na mchezo wake dhidi ya Nigeria siku ya Jumamosi Septemba 5,
2015 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwania kufuzu kwa
fainali za Mataifa Afrika mwaka 2017.
Kocha Mkuu wa Stars Charles Mkwasa akiongea na tovuti rasmi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) www.tff.or.tz amesema anashukuru kambi imekua na mafanikio makubwa kwani vijana wanaonyesha mabadiliko makubwa sana.
“Ukiondoa
mchezaji moja tu ambaye ni majeruhi Abdi Banda, Mkwasa amesema
wachezaji wengine wote wapo fit na kila mmoja atakayepata nafasi katika
mchezo wa sikuya jumamosi atafanya vizuri” amesema Mkwasa.
Mkwasa
amesema mazingira ya kambi yamekua mazuri, na katika mechi ya maozezi
dhidi ya Libya iliyochezwa siku ya ijumaa, vijana wake walicheza vizuri
kwa nguvu na kufuata maelekezo yake, makosa machache yaliyojitokeza
katika mchezo huo wameyafanyia kazi na sasa anaamini wako tayari
kuwakabili Nigeria.
Mwisho
Mkwasa amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa siku
ya jumamosi kuishangilia timu ya Taifa, kwani uwepo wa washabiki wengi
uwanjani utawaongeza morali zaidi wachezaji na kujiona wapo nyumbani
wanapambana kwa ajili ya Taifa lao.
Naye
nahodha wa Taifa Stars, Nadir Haroub “Cannavaro” amesema maandalizi
waliyopata ni mazuri na yamewajenga vilivyo kuelekea kwenye mchezo dhidi
ya Nigeria siku ya jumamosi na kuwaomba watanzania kuja kwa wingi
kuwasapoti.
Nadir
amesema wao kama wachezaji kila mmoja yupo fit na anahitaji kucheza
mechi hiyo, hivyo yeyote atakayepata nafasi ya kucheza ana imani
atafanya vizuri katika kuipeperusha bendera ya Tanzania.
Stars
ambayo iliweka kambi ya takribani siku nane katika milima ya Katrepe -
Kocaeli, inatarajiwa kuodoka kesho jumanne saa 1 jioni nchini Uturuki
kurejea nyumbani kwa usafiri wa shirika la Ndege la Uturuki (Turkish
Airlines) na kuwasili uwanja wa JK Nyerere majira ya saa 9 kasoro usiku.
Mara
baada ya kuwasili Dar es salaam timu itaendelea na kambi kwa kufanya
mazoezi mepesi siku ya jumatano pamoja wa wachezaji wa kimataifa Mbwana
Samatta, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngasa katika uwanja wa Taifa
kujiandaa na mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya Nigeria
Post a Comment