SITTA AMJIBU SUMAYE KUHUSU MABEHEWA MABOVU


Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Sitta akisisitiza jambo.
Wanahabari wakichukua matukio katika hafla hiyo.
Wanahabari wakifuatilia tukio.
WAZIRI wa Uchukuzi, Samwel Sitta, amemjibu Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, baada ya kuituhumu serikali ya Rais Kikwete kuwa imewafumbia macho watendaji walioisababishia hasara nchi zaidi shilingi bilioni 220 kwenye ununuzi wa mabehewa yanayotajwa kuwa ni feki.
Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za wizara yake, Sitta amesema watendaji wote waliohusika na kashfa hizo watafikishwa mahakamani muda wowote kutoka sasa baada uchunguzi kukamilika.
Aliongeza kwamba kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo imeshakamilisha kazi yake na kuonesha kulikuwa na uzembe kwa watendaji wa shirika la reli (TRL) uliosababisha kununuliwa kwa mabehewa hayo.
Aidha amesema kuwa kamati hiyo ilikwenda hadi nchini India kuichunguza kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industrial Limited ambayo ndiyo watengenezaji wa mabehewa hayo mabovu na kubaini kampuni hiyo iliyopewa zabuni ilikuwa haina sifa.
Hata hivyo, Sitta ameongeza kuwa kamati hiyo ilibaini kampuni hiyo haikuwa na sifa na watendaji TRL walikiuka kanuni za manunizi ya serikali kwa kitendo chao cha kutoa fedha zote kwa kampuni hiyo kabla hawajaleta mabehewa.
Viongozi wanaotuhumiwa katika sakata hilo kuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Kipallo Kisamfu; Mhandisi Mkuu wa Mitambo, Ngosowile Ngosomiles; Mhasibu Mkuu Mbaraka Mchopa; Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Kampuni, Jasper Kisiraga; na Meneja Mkuu wa Manunuzi, Ferdinand Soka.
(NA DENIS MTIAMA/GPL)

Post a Comment

Previous Post Next Post