WAGOMBEA CCM WAPINGA USHINDI WA NAPE MNAUYE (MTAMA) NA SAID MTANDA (MCHINGA)


uchaguzi wa ubunge ccm lindi
Makada wa Chama cha Mapinduzi ambao walikuwa wagombea nafasi ya Ubunge kura za maoni Kupitia CCM kutoka katika Majimbo ya Mtama na Mchinga Lindi, wakiwa katika Press Conference na waandishi wa Habari Mkoani lindi katika Hoteli ya Lindi Oceanic. 
uchaguzi wa ubunge ccm lindi
Mwenyekiti wa wagombea akiongea na Waandishi wa habari wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari baada ya kutolewa kwa Matokea ya Chama cha Mapinduzi kwa nafasi za Ubunge na Udiwani katika Majimbo ya Mtama na Mchinga. 
uchaguzi wa ubunge ccm lindi
Mgombea wa Nafasi ya Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi Riziki Lulida akionesha Moja ya kitabu cha karatasi za Kupigia kura ambavyo alibainisha kuwa vilikuwa vimezagaa katika sehemu ya kupigiakura kinyume na Utaratibu.

Na. Mwandishi Wetu, Lindi
Wagombea waliokuwa wakiwania Kukiwakilisha Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya Ubunge katika Majimbo ya Mtama na Mchinga wameweza kueleza masikitiko yao dhidi ya wagombea wenzao wawili ambao wametangazwa kuwa wao ndio washindi katika maeneo hayo mawili ambao kwa Jimbo la Mtama alietangazwa ni Nape Mnauye ambaye aliweza kufuatwa kwa karibu na Mgombea Seleman Methew, Kwa jimbo la Mchinga Said Mtanda ametangazwa kuwa Mshindi Huku akifuatiwa na Mebu.

Kufuatia Matokeo hayo yaliyoweza kutangazwa na Chama hicho katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Mkoa Lindi, wagombea hao wameeleza kutoyakubali matokeo hayo kwani wamebainisha kuwa kuna Udanganyifu mkubwa umetumika, Lalamiko la kwanza lililotolewa na wagombea hao ni Kutopatiwa Akidi ya wanachama kabla ya Kupiga kura, La pili ni Mgombea kusafirisha watu kutoka eneo moja kupeleka eneo jingie kwa ajili ya kupiga kura na Jambo la tatu kuongeza karatasi za kupigia kura ambazo tayari zimesha pigwa tiki katika masanduku ya kupigia kura.


Wagombea hao wameongeza yakuwa wapiga kura wengine waliopiga kura si wa wanachama wa Chama cha Mapinduzi ni wanachama cha wananchi (C.U.F) na wamebainisha Ushahidi wanao. Hivyo kufuatia matukio hayo wagombea hao wameweza kubainisa kuwa Uleusemi wa Katibu Uenezi wa Chama hicho alioutoa siku kadhaa zilizopita kuwa CCM itashinda kwa kishindo hata kwa Goli la Mkono limeweza kutimia kwani mazingira ya Ushindi wake katika Jimbo la Mtama umegubikwa na Udanganyifu mkubwa.

Kufuatia Udanganyifu huo wa wagombea hao wameweza kubainisha kuwa hawako tayari kuwaunga mkono wagombea hao waliotangazwa na Chama hicho kama washindi na kusema kama Chama kitakuwa sikivu basi Uchaguzi huo Urudiwe la sivyo wao hawakotayari kuwaunga mkono katika Uchaguzi Mkuu.

Aidha Mgombea aliyeshika nafasi ya pili katika jimbo la Mtama ameweza kutoa rai ya kuwa CCM kama itaruhusu hali hii inayoendelea kwa sasa basi ni dhahiri kuwa chama hicho kiko mbioni kupotea kwani wanachama wake wa ngazi za juu wanatumia Udanganyifu mkubwa kupata nafasi za uongozi hususani kutoa rushwa na kutengeneza karatasi za kupigia kura zisizo rasmi.

CHANZO: LINDI YETU

Post a Comment

Previous Post Next Post