Makada
wa Chama cha Mapinduzi ambao walikuwa wagombea nafasi ya Ubunge kura za
maoni Kupitia CCM kutoka katika Majimbo ya Mtama na Mchinga Lindi,
wakiwa katika Press Conference na waandishi wa Habari Mkoani lindi
katika Hoteli ya Lindi Oceanic.
Mwenyekiti
wa wagombea akiongea na Waandishi wa habari wakati wa Mkutano na
waandishi wa Habari baada ya kutolewa kwa Matokea ya Chama cha Mapinduzi
kwa nafasi za Ubunge na Udiwani katika Majimbo ya Mtama na Mchinga.
Mgombea
wa Nafasi ya Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi Riziki Lulida akionesha
Moja ya kitabu cha karatasi za Kupigia kura ambavyo alibainisha kuwa
vilikuwa vimezagaa katika sehemu ya kupigiakura kinyume na Utaratibu.
Na. Mwandishi Wetu, Lindi
Wagombea waliokuwa wakiwania Kukiwakilisha Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya Ubunge katika Majimbo ya Mtama na Mchinga wameweza kueleza masikitiko yao dhidi ya wagombea wenzao wawili ambao wametangazwa kuwa wao ndio washindi katika maeneo hayo mawili ambao kwa Jimbo la Mtama alietangazwa ni Nape Mnauye ambaye aliweza kufuatwa kwa karibu na Mgombea Seleman Methew, Kwa jimbo la Mchinga Said Mtanda ametangazwa kuwa Mshindi Huku akifuatiwa na Mebu.
Kufuatia Matokeo hayo yaliyoweza kutangazwa na Chama hicho katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Mkoa Lindi, wagombea hao wameeleza kutoyakubali matokeo hayo kwani wamebainisha kuwa kuna Udanganyifu mkubwa umetumika, Lalamiko la kwanza lililotolewa na wagombea hao ni Kutopatiwa Akidi ya wanachama kabla ya Kupiga kura, La pili ni Mgombea kusafirisha watu kutoka eneo moja kupeleka eneo jingie kwa ajili ya kupiga kura na Jambo la tatu kuongeza karatasi za kupigia kura ambazo tayari zimesha pigwa tiki katika masanduku ya kupigia kura.
Wagombea hao wameongeza yakuwa wapiga kura wengine waliopiga kura si wa wanachama wa Chama cha Mapinduzi ni wanachama cha wananchi (C.U.F) na wamebainisha Ushahidi wanao. Hivyo kufuatia matukio hayo wagombea hao wameweza kubainisa kuwa Uleusemi wa Katibu Uenezi wa Chama hicho alioutoa siku kadhaa zilizopita kuwa CCM itashinda kwa kishindo hata kwa Goli la Mkono limeweza kutimia kwani mazingira ya Ushindi wake katika Jimbo la Mtama umegubikwa na Udanganyifu mkubwa.
Kufuatia
Udanganyifu huo wa wagombea hao wameweza kubainisha kuwa hawako tayari
kuwaunga mkono wagombea hao waliotangazwa na Chama hicho kama washindi
na kusema kama Chama kitakuwa sikivu basi Uchaguzi huo Urudiwe la sivyo
wao hawakotayari kuwaunga mkono katika Uchaguzi Mkuu.
CHANZO: LINDI YETU
إرسال تعليق