- Mbatia analalamikia vitisho vya Mgombea wa CCM, Magufuli kuwa wakiwachagua wapinzani nchi itaingia kwenye machafuko
- Mbatia: Watu wameanza kupoteza maisha, wana UKAWA wanadhalilishwa na wengine kutekwa
- Mbatia: Hali imeanza kuwa tete, vitisho vya kila aina vimeanza. Tumedhalilishwa sana, tumeitwa matusi ya kila aina.
-
Mbatia: Lowassa si mdini, alikuwa anataka watanzania wamwombee. Mhe.
Lowassa hajaenda kwenye nguvu za giza. Hajatumia viungo vya albino,
ameenda kuomba viongozi wa dini wamwombee; udini wake unatoka wapi?
- Mbatia: Tunawashukuru Lowassa na Sumaye kwa nia zao njema kuja Upinzani kuongeza nguvu ili tuyafanye mabadiliko ya kweli
- Mbatia: Hata CCM wangemweka malaika, si rahisi kupata mabadiliko bila kufanya mabadiliko ya mfumo.
-
Mbatia: CCM wanasema usichague chama, chagua mtu. Watanzania wanatakiwa
kujua kuwa Magufuli ni CCM, na hawezi kujitenganisha na CCM. Huwezi
kulisukuma gari ukiwa ndani yake, lazima utoke ndipo ulisukume.
Mabadiliko ndani ya CCM hayawezekani
- Mbatia: Tumefanya utafiti, tuna uhakika wa ushindi mwaka huu
- Mbatia: Hatutawapa CCM nafasi ya kufanya machafuko ndani ya Taifa hili
- Mbatia: CCM hawana hati miliki ya kuitawala Tanzania hii. Watupishe tufanye mabadiliko haya kwa utulivu na amani.
-
Mbatia: Sumaye, Lowassa wana uzoefu mkubwa wa kuongoza Serikali, uwezo
tunao! Tunao kina Mungai, Msindai, Mgeja n,k na wanao uzoefu wa kuongoza
Serikali.
- Mbatia: Limeibuka suala la ukabila. Ni aibu iliyoje? CCM wanahubiri ukabila, ukanda bila aibu yoyote!
-
Mbatia: Ilani ya Uchaguzi ni mkataba kati ya mpiga kura na mpigiwa
kura; tuwaulize CCM Ilani yao iliyopita imetekelezwa kwa kiasi gani
kabla hawajaja na ilani mpya. UKAWA tunayo ilani ya pamoja
- Mbatia: Tunawataka CCM waje tufanye midahalo kwa hoja
- Mbatia: Wenyeviti wa vyama wawekwe kwenye midahalo ili UKAWA tupambane na CCM kwa hoja na watanzania wajue pumba na mchele
- Mbatia: UKAWA ipo imara, haitasambaratika!
- Mbatia anafafanua wapi watapata fedha za kufanikisha yale wanayoahidi kwenye kampeni.
- Mbatia anadai Safari za Rais hazikuwa na tija kwa Taifa.
- Mbatia: Lowassa na Serikali yake wakiingia madarakani wanao uwezo wa kupunguza kodi kwa wafanyakazi
- Mbatia: Tukinyimwa haki yetu kwa mbinu chafu… Hatutaki kuona yaliyotokea Kenya yakitokea Tanzania |
إرسال تعليق