THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Alhamisi, Septemba 10, 2015 amepokea tuzo nyingine ya kimataifa, siku mbili tu baada
ya kupokea tuzo ya kutambua mchango wake katika kudumisha amani na utulivu katika
Tanzania.
Rais
amekabidhiwa tuzo hiyo ya Uongozi na Utawala Bora na Waziri wa Katiba na Sheria,
Mheshimiwa AshaRose Migiro ambaye aliipokea kwa niaba ya Rais Kikwete katika sherehe
iliyofanyika Julai 25, mwaka huu, 2015, Afrika Kusini.
Rais
Kikwete ametunukiwa tuzo hiyo na Bodi ya Uongozi ya Africa Archiever’s Award kwa kutambua mchango wake katika maeneo ya
uongozi na utawala bora wakati wa uongozi wake wa miaka 10 wa Tanzania.
Hafla
ya makabidhiano hayo imefanyika Ikulu, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi
mbalimbali, miongoni mwa viongozi waliohudhuria, ni Katibu Mkuu Kiongozi (KMK)
Balozi Ombeni Yohana Sefue, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu George Masaju,
Kaimu Katibu Mkuu Ikulu Ndugu Susan Mlawi na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu
na Utawala Bora Ndugu Tom Bahame Nyanduga.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi tuzo hiyo,Waziri Migiro amesema kuwa kwa kupata tunuku hiyo sasa
Rais Kikwete anajiunga na waafrika wengine mashuhuri ambao wamepata tuzo hiyo ambao
ni Rais wa zamani wa Ghana, Hayati John Atta Mills, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja
wa Afrika Mama Nkozana Dlamini Zuma na aliyekuwa kiongozi wa Kanisa la Anglikana
na Duniani na mwanaharakati mashuhuri waAfrika, Askofu Mkuu Desmond Tutu.
Waziri
Migiro amesema kuwa Rais Kikwete alikuwa miongoni mwa Waafrika mashuhuri 1,202
ambao majina yao yalipendekezwa kwa ajili ya kutunukiwa tuzo hiyo kwa mwaka huu
lakini Bodi iliyomtunukia Rais Kikwete tuzo hiyo imeridhishwa zaidi na mchango wake
mkubwa katika kujenga na kuleta utawala bora katika miaka yake 10 ya uongozi wa
Tanzania.
Amesema
kuwa miongoni mwa vigezo vikuu vya tunuku hiyo ni jinsi Rais Kikwete alivyosimamia
utawala wa sheria, alivyochangia kujenga demokrasia nchini, uongozi wake
ulivyopambana na rushwa, ulivyoheshimu haki za binadamu, ulivyokuwa stahimilivu
na ulivyoinua uhuru wa kila aina nchini.
Waziri
Migiro pia amezungumzia maudhui ya mada ambayo Rais Kikwete aliitoa baada ya kutunukiwa
tuzo hiyo ambayo kichwa chake cha habari kilikuwa African Unity: Prospects and
Challenges (Umoja wa Afrika: Fursa na Changamoto) ambako miongoni mwa
mambo mengine Rais alithibitisha uhusiano kati ya ustawi ama umasikini na utulivu
katika Bara la Afrika.
Rais
pia alizungumzia kuhusu hamu yake ya kustaafu baada ya kumaliza ngwe ya uongozi
wake, akisisitiza kuwa hiyo ni sehemu ya utamaduni na ustawi wa demokrasia ya
Tanzania na kuwa kwa sababu ya uvumilivu wa uongozi hakuna Rais yoyote wa
Tanzania amepata kulazimika kukimbia nchi kwenda kuishi uhamishoni.
Naye
Rais Kikwete amesema kuwa hakuweza kwenda mwenyewe kupokea tuzo hiyo kwa sababu
wakati huo alikuwa katika ziara rasmi ya Kiserikali katika Australia lakini akaongeza
kuwa amefurahi kutunukiwa tuzo hiyo.
Amesema
kuwa tunuku hiyo ni ya Watanzania na yeye ameipokea tu kwa niaba yao na kwa niaba
ya Serikali yake ambayo ndiyo imechangia kuboresha utawala bora chini ya uongozi
wake.
“Mimi
naipokea tuzo hii kwa niaba ya Watanzania. Wao ndio washindi wa kwelikweli wakiongozwa
na Serikali yao ambayo imefanikisha kudumisha utawala bora katika miaka 10
iliyopita.Wenzetu wametupima kwa kutulinganisha na wengine na tukaonekana bora.
Nawashukuru sana kwa imani yao kwetu.”
Tuzo
hiyo ya Uongozi na Utawala Bora imekuja siku mbili baada ya Rais kupokea Nishani
ya Amani na Utulivu iliyotolewa kwake na Taasisi ya East Africa Book Records
yenye makao makuu yake Uganda na kukabidhiwa kwa Rais Kikwete na mtendaji wake
mkuu, Dkt. Paul Bamutize.
Akitunuku
nishani hiyo juzi, Jumanne, Septemba 8, 2015 katika hafla nyingine iliyofanyika
Ikulu, Dar es Salaam, Dkt. Bamutize alisema kuwa amani na utulivu ambao Rais Kikwete
na Serikali wamejenga katika Tanzania imeleta matumaini kwa wawekezaji na majirani
wa Tanzania na kuwa mfano dhahiri wa kuigwa.
Hafla
hiyo ilihudhuriwa na mabalozi wa Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo (DRC).
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
10 Septemba, 2015
إرسال تعليق