‘MUUZA nyago’ kupitia muziki na
filamu hapa Bongo, Isabella Mpanda amekwaa skendo ya kuuza wasichana kwa
mapedeshee, kufuatia jina lake kutumiwa na mtu ambaye jina lake halisi
halikupatikana mara moja, ambaye anajitambulisha kwa jina la msanii
huyo.
Mpashaji wa habari hii ambaye ni rafiki
wa karibu na Isabella aliliambia gazeti hili kuwa, mhalifu huyo wa
mtandaoni, anatumia picha ya Isabella kuwataka wanaume wenye pesa
wamuone na yuko tayari kuwaunganisha kwa wasichana wazuri wa mjini.
Isabella alipoulizwa juu ya habari hiyo
alikiri kukumbana na kadhia hiyo, ambapo alisema: “Nimempata huyo mtu,
anaitwa Angel, nilimpigia simu akaniomba msamaha akidai kuwa njaa
imemsukuma kufanya hivyo, nimemsamehe lakini kwa onyo kali la kutorudia
upuuzi wake huo.”

إرسال تعليق