NENO mafanikio lina maana pana sana na kwa mujibu wa wanasaikolojia, tafsiri sahihi ya neno hilo hubadilika kati ya mtu na mtu anayelihubiri au kuliishi.
Katika mfano mmoja wa kuchekesha sana,
bosi wangu aliwahi kusema wapo baadhi ya watu, kuzungumza na mastaa
wakubwa ni ndoto za maisha yao, kwa maana hiyo, hayo ndiyo mafanikio
yao!
Maana
nyepesi hapa ni kuwa mafanikio yako, siyo ya yule kwa sababu ndoto
zinatofautiana. Unaweza kumuona mtu analala chini katika mabaraza ya
majumba makubwa mtaa wa Samora, jijini Dar es Salaam ukawa unamhurumia,
lakini kwake yeye, hayo ndiyo maisha bora kabisa ya ndoto zake, tofauti
na kwao Mkumbi alikotoka!
Nimeanza hivi ili kujaribu kuzungumza na
msanii mwenye jina kubwa kwa sasa hapa nchini, Diamond Plutnamz. Majuzi
alirejea kutoka Marekani akiwa na tuzo tatu za Afrimma alizotwaa, akiwa
mbele ya wenzake Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz, waliopata tuzo moja moja.
Baada ya kupokewa na mamia ya mashabiki
wake uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, msafara wao uliishia Escape One,
ambako pamoja na kuzungumza nao, pia kulikuwa na burudani ya muziki. Ni
katika mazungumzo yake, ndipo nilipopata wazo la kusema naye kwenye
safu hii.
Diamond aliwaambia wanahabari kuwa
wasanii wa Tanzania wanamuonea wivu kutokana na maendeleo yake kimuziki,
ndiyo maana hakukuwa na yeyote aliyejitokeza kumuunga mkono siku hiyo,
licha ya ukweli kuwa tuzo alizopata, sifa ni kwa Watanzania wote!
Kwanza nikiri kuwa mimi ni mmoja wa watu
wanaofurahia jinsi Diamond anavyojitengenezea thamani katika muziki
wake. Anajitahidi kufanya kila kitu kwa ubora, kuanzia uimbaji, madansa
wake, video zake na mengineyo, kiasi cha kuwaaminisha wasanii wa nje
kuwa yeye ndiye msanii bora kuliko wote Tanzania.
Hili ni jambo zuri, kwa sababu katika
muziki wa biashara yenye ushindani kama wa sasa ulivyo, ubunifu ni kitu
cha muhimu sana. Lakini hili la wivu kidogo linanitatiza.
Ninachojua mimi, Wabongo hatupendani,
siyo kwa wasanii tu, bali hata wananchi wa kawaida mitaani. Na hali
inakuwa mbaya zaidi unapoonesha dalili za kusogea kutoka hatua moja
kwenda nyingine nzuri zaidi.
Lakini najiuliza, Diamond amefanikiwa
kweli kwa kiasi gani hadi achukiwe na wenzake? Maana kuna tatizo pia,
Mbongo mwenye mafanikio wenzake wakijitokeza kumuunga mkono, anabadilika
na kujiona anapapatikiwa!
Ni kweli kwamba Diamond amekamata mpini
miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva kwa umaarufu kwa sasa, lakini
unadhani hakuna watu wanapiga hela kuliko yeye?
Kuna watu tunawajua wana miradi mingi
iliyotokana na muziki, ambao huenda akaunti zao zinasoma kuliko
tunavyofikiri, je, hawa nao wanamuonea wivu?
Dogo analo la kujifunza hasa kuhusu
kauli anazozitoa mbele ya hadhara. Kama anadhani kuna siku wasanii
wenzake watajikusanya na kumsifu kwamba yeye ndiye dira yao, naamini
atasubiri sana kwa sababu siku hiyo haitatokea.
Anachopaswa kufanya ni kuendelea kupiga kazi na kuwaacha mashabiki waamue kuhusu nani ni nani.
Dawa ya Wabongo ni kuziba masikio na
kufumba macho unapofanya mambo yako, ukitaka usikie wanachosema juu
yako, au wanachokiona kwako, utaishia maumivu.
Maisha ya kusikilizia sifa yamepitwa na
wakati, maana kama nilivyosema pale mwanzo, mastaa wa Kibongo kila mmoja
anajiona yupo juu
إرسال تعليق