Gari yagonga mnazi huko kibele Unguja na kuukata, waangukia gari dereva apona


Dereva wa gari hili Z 511 FG  ambaye inaaminika ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) (jina halikupatikana) ameponea chupuchupu baada ya mifumo ya usalama ya gari hili ilipofanikiwa kufyatua puto mara tu baada ya gari hili kukosa mwelekeo na kugonga mnazi.Ajali hii imetokea katika kijiji cha Kibele, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja na inaaminika kuwa dereva huyo alishindwa kuidhibiti gari ndogo aina ya Toyota Spacio kutokana na mwendo kasi ambayo ilihama barabarani  na kugonga mnazi ambao uliangukia gari na baadae gari kuwaka moto.
Dereva alitolewa ndani ya gari akiwa amebanwa na puto (air bags)  zilizofyatuka na kuokoa uhai wake. Alipata majeraha madogo ya kuchubuka kwenye mikono yake iliyokuwa inavuja damu. 

No comments:

Post a Comment