Gwajima Amkana Edward Lowassa.....Adai Yeye Hakuwahi Kumuunga Mkono Wakati Wa KampeniMchungaji wa kanisa la ufufuo na uzima,Josephat Gwajima amejitokeza hadharani  na kukana kwamba hakuwahi kumuunga mkono Edward Lowassa wakati wa kampeni za Urais.

Akiongea katika mahojiano maalumu na kituo cha Azam Tv, Gwajima amesema yeye hakuwahi kuwa mshirika wa Lowassa wala chama chochote, bali aliitwa jijini Arusha na Jangwan Dar es Salaam  kwa ajili ya maombi tu na sivinginevyo....

Amesema kitendo cha kukubali wito huo wa maombi kimewafanya watanzania wahisi kwamba yeye alikuwa team Lowassa, kitu ambacho sio kweli.

Amedai yeye alikuwa mfuasi wa mabadiliko ya nchi, alikuwa akiunga mabadiliko ya nchi na SIO  personality ya mtu au chama cha mtu.

Wakati Gwajima akikana kumuunga mkono Lowasaa, kumbukumbu zinaonyesha kuwa mchungaji huyo alikuwa ni team Lowassa na  alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha mheshimiwa Lowassa anashinda kiti cha Urais.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Gwajima alitumia nguvu kubwa sana wakati wa kampeni kupambana na Dr Slaa ambaye wakati huo alikuwa akishusha makombora mazito kuhakikisha Lowassa hashindi huku akimtuhumu Gwajima kuwa mshenga wa Lowassa aliyemfuata kumpigia debe wampokee Chadema

Tazama Video hii Kumsikiliza GwajimaBaada ya Mchangaji Gwajima Kumkana Lowassa, nimelezimika  kuitafuta Video ya Maombi ya Gwajima tarehe 29.08.2015 Jangwani, Dar es Salaam wakati UKAWA Walipokuwa wakizindua kampeni zao.
Miongoni mwa maneno aliyoyasema Gwajima siku hiyo ni kuwa Anayemlaani Lowassa  na Haji Duni, Laana iwarudie wenyewe kwa kuwa huu ni wakati wa Lowassa na hakuna wa kumzuia. Je, ni Kweli Gwajima hakuwa mshirika wa Lowassa kama alivyomkana leo?
Tazama video hapo chini


No comments:

Post a Comment