Jack Patrick kilio upya akiwa gerezani!JACK Patrick, msanii, mwanamitindo na mmoja wa Watanzania wanaotumikia kifungo nchini China kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya, ametoa kilio upya akiwa gerezani, baada ya kuwashutumu marafiki zake kushindwa kumtembelea, licha ya kufika mara kwa mara katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa barani Asia.

Kikizungumza na gazeti hili juzikati, chanzo kilichoomba hifadhi ya jina lake, ambacho kilimtembelea Jack katika gereza lililo mji wa Maccau, kilisema msanii huyo licha ya kuumizwa na mambo mengi, lakini usaliti unaofanywa na marafiki zake wa karibu ndiyo unamuuma zaidi.

“Jack alitarajia watu wake wa karibu aliokula nao bata wakati wa furaha wangeenda kumtembelea mara kwa mara akiwa gerezani, lakini badala yake imekuwa kinyume licha ya kuishi kama ndugu kipindi cha nyuma.

“Badala yake wanaomtembelea ni watu ambao hakuwahi kuwa nao karibu kabla, hili linamuuma sana na ameahidi akitoka atajitafakari upya urafiki wake na watu hao,” kilisema chanzo chetu kikimnukuu msichana huyo aliyehukumiwa mwaka 2013 kwenda jela miaka sita.

No comments:

Post a Comment