Co- founder wa Pop Up Bongo
Natasha Stambuli akionesha bidhaa za duka lake la Secret Habit ambalo
nalo lilionesha bidhaa zake siku hiyo.
Andrew Mahiga na rafiki ake walikuwapo.
Mmoja kati ya wanawake wajasiriamali mahiri mjini, Aika Lawere mmiliki wa Mbezi Garden alikuwapo pia.
Mbunifu
wa mavazi nchini wa lebo ya Branoz Collection, Bahati Kombe (katikati)
akipanga bidhaa zake wakati wa Tamasha la Pop Up Bongo lililofanyika
juzi Triniti Oysterbay chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff.
Meneja
chapa (pombe kali) wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija,
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Wauzaji
wa bidhaa mbalimbali kutoka duka la Beauty Haven wakiwa kwenye banda
lao wakati wa Tamasha la Po Up Bongo lililofanyika juzi Triniti Oyster
bay chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff
Atu Mynah akimtaja mshindi wa bahati nasibu siku hiyo.
Kutokea banda la Beauty Heaven kulikuwa na bidhaa mbalimbali pia.
Natasha akizungumza na mmoja kati ya washiriki waliojitokeza kuonesha bidhaa siku hiyo.
ONESHO la
mauzo ya bidhaa mbalimbali zitengenezwazo na wabunifu wa hapa nchini,
Pop Up Bongo lilifanyika hivi karibuni na kuhudhuriwa na watu
mbalimbali.
Mratibu wa
onesho hilo lililofanyikia Triniti Oyster bay,Natasha Stambuli alisema
kuwa zaidi ya wajasiriamali 15 walijiotokeza kuonesha na kuuza bidhaa
zao.
Alisema
kuwa bidhaa mbalimbali kama vile nguo, vito, viatu na vinginevyo
viliuzwa na wajasiriamali hao walipata wasaha wa kuongeza wigo wao
kibiashara kwa kukutana na wanunuzi.
“Pop Up
Bongo inalenga kuwaweka karibu zaidi wajasiriamali na wanunuzi hao kwa
kuwakutanisha mahala hapa na kisha hata wakishafanya mauzo wanakuwa na
wasaha wa kuonana hata baada ya Tamasha hili na kuendeleza uhusiano wa
kibiashara” alisema Natasha.
Pia ametoa
wito kwa wanajamii kujenga utamaduni wa kuhudhuria maonesho mbalimbali
ya biashara ili kupanua wigo zaidi wa ufahamu wa aina mbalimbali za
bidhaa ziuzwazo nchini.
Natasha
alisema kuwa kwa kutembelea maonesho hayo watapata wasaha wa kufahamu
aina mbalimbali za bidhaa ziuzwazo na wafanyabiashara mbalimbali na
kujua ni wapo pa kwenda kujipatia mahitaji.
Alisema
kuwa Pop Up Bongo ikiwa chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff
inalenga kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali
zitengenezwazo hapa nchini na wanunuzi kwa lengo la kuwasaidia
wajasiriamali wa hapa nchini kuongeza pia wigo wa biashara zao.
Kwa upande
wake Meneja chapa (pombe kali) wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)
Shomari Shija, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
alisema kuwa kwa kampuni hiyo inatambua nafasi ya wajasiriamali katika
kuendeleza uchumi wa nchi na ndio maana imeamua kuunga mkono Pop Up
Bongo.
“SBL kwa
kupitia kinywaji chetu cha Smirnoff tumeamua kudhamini Pop Up Bongo kwa
kuwa ni mahala pazuri kwa wapenzi wa kinywaji hiki kukutana huku
wakijipatia mahitaji yao kadhaa kutoka kwa wauzaji wanaouza bidhaa zao
katika Pop Up Bongo” alisema Shomari
Post a Comment