Saudi
Arabia imesema nchi 34 zimekubaliana kuunda muungano wa kijeshi wa
kiislamu kupambana dhidi ya ugaidi ambapo operesheni za pamoja zitakuwa
zikiratibiwa kutoka mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.
Tangazo
hilo limechapishwa na shirika la habari la Saudi Arabia na kuongeza
muungano huo utaongozwa na nchi hiyo na umeanzishwa kwa sababu ugaidi
unapaswa kukabiliwa kwa kutumia kila njia na ushirikiano huo utakuwa
njia mwafaka utakao uangamiza.
Taarifa
hiyo inasema Uislamu unapinga ufisadi na maangamizi na ugaidi unakiuka
hadhi na haki za binadamu hasa haki ya kuishi na kuwa salama. Miongoni
mwa nchi zitakazoshiriki katika muungano huo ni Pakistan, Uturuki,
Misri, Libya na Yemen. Mali, Chad, Somalia na Nigeria pia ni wanachama
wa muungano huo mpya wa kupambana dhidi ya ugaidi.
Hasimu wa
muda mrefu wa Saudi Arabia, Iran haijajumuishwa katika muungano huo.
Saudi Arabia na Iran zimekuwa zinayaunga mkono makundi tofauti katika
mizozo ya Yemen na Syria. Oman pia haijashirikishwa katika muungano huo
wa kijeshi.(P.T)
Asasi za kimataifa zitashirikishwa
Katika
mkutano na wanahabari, mwana wa mfalme wa Saudi Arabia ambaye ni waziri
wa ulinzi Mohmmed bin Salman amesema muungano huo wa kijeshi wa nchi za
kiislamu utaunda mfumo wa kushirikiana na nchi nyingine na asasi za
kimataifa katika kuunga mkono juhudi za kupambana na ugaidi na kwamba
hawajikita tu katika kulikabili kundi la wanamgambo wenye itikadi kali
wa dola la kiislamu IS. Mwanamfalme huyo amesema kitisho cha ugaidi ni
kikubwa
''Leo
kuna mataifa kadhaa yanayokumbwa na ugaidi, kwa mfano Dola la Kiislamu
nchini Syria na Iraq, ugaidi Sinai, ugaidi Yemen, ugaidi Libya ugaidi
Mali, ugaidi Nigeria, ugaidi Pakistan, ugaidi Afghanistan na hili
linahitaji juhudi thabiti ili kupambana nao'' Amesema mwanamfalme
Salman, na kuongeza kuwa Bila shaka kutakuwa na ushirikiano katika
juhudi hizo.
Kama Iran, Oman pia yatengwa
Mataifa
wanachama wa muungano huo ni pamoja na taifa dogo la Maldives na taifa
la kisiwani cha Bahrain katika Ghuba ya wajemi ya kiarabu, ambayo pia ni
makao makuu ya jeshi la majini la Marekani. Mataifa mengine ya ghuba
ambayo yameshirikishwa katika muungano huo ni Kuwait,Qatar na falme ya
milki za kiarabu. Oman ambayo ni jirani ya Saudi Arabia haipo katika
muungano huo. Siku za hivi karibuni Oman imekua ikishikilia msimamo wa
wastani kama mpatanishi katika mzozo wa mashariki ya kati.
Wanachama
wote wa muungano huo pia ni sehemu ya Shirika kubwa ya Ushirikiano wa
Kiislamu, ambayo makao yake makuu yako nchini Saudi Arabia. Uturuki ndio
mwanachama wa pekee wa shirika la kujihami la Nato kujiunga na Muungano
huo.
Mwandishi: Ambia Hirsi/APE/
Mhariri: Daniel Gakuba
Chanzo:DW
Post a Comment