MKUU
WA MKOA WA DAR ES SALAAM ATOA TAMKO NA KUSEMA SHERIA NA KANUNI ZA NCHI
LAZIMA ZIFUATWE, MIHADHARA IMESIMAMISHWA MPAKA HALI ITAKAPOKUWA SALAMA
NA JESHI LA POLISI LIMEJIPANGA VEMA KATIKA KUKABILIANA NA VURUGU
ZITAKAZOJITOKEZA.
Na Adrophina Ndyeikiza-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa DSM 19/10/2012
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki amekutana na waandishi wa
habari leo asubuhi katika Ofisi yake na kutoa tamko kuhusu vurugu
zinazoendelea kujitokeza katika Mkoa wa Dar es Salaam. Mhe.Mkuu wa
Mkoa amesema kuwa kumeibuka vitisho vya hapa na pale katika Mkoa wa Dar
es Salaam baada ya kukamatwa kwa Sheikh Issa Ponda ambaye anajulikana
kama Katibu wa Baraza kuu na Taasisi za Jumuiya ya Kiislamu. “Mpaka sasa
wametoa taarifa kuwa kutakuwepo na maandamano ya kuelekea Ikulu ili
kushinikiza kuachiwa huru kwa Sheikh Issa Ponda na wafuasi wake”.Alisema
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Maandamano hayo hayana kibali chochote
kile ni kutaka kuibua vurugu na uvunjifu wa amani kwa wana Dar es
Salaam,hivyo basi nawaomba wananchi wa Dar es Salaam kutokushiriki
katika maandamano hayo kwani kwa kufanya hivyo sheria kali zitachukuliwa
dhidi ya waandamanaji kwani maandamano hayo ni Haramu na hayana kibali
wala tija kwa Taifa letu.Alisisitiza Mkuu wa Mkoa. Aidha,Mkuu wa Mkoa
alisema kuwa lazima tufike mahali tuishi kwa kufuata misingi ya taratibu
na sheria za taifa letu kwani Sheikh Ponda hakukamatwa kama Sheikh bali
kama mchochezi wa vurugu na kuwashawishi wafuasi wake kuidharau
Serikali na vyombo vya usalama.Hivyo amekamatwa kama mtuhumiwa mwingine
yoyote anayeweza kukamatwa. Hivyo basi yatupasa tuwe na subira na
kufuata taratibu husika kwani kama Sheikh Issa Ponda hana hatia basi
ataachiwa na kama ana hatia basi atahukumiwa kama ilivyo kawaida kwa
mtuhumiwa yoyote yule akipatikana na hatia.Hivyo basi lazima tujue kuwa
nchi yetu inaongozwa kwa misingi ya taratibu na sheria na hakua aliye
juu ya sheria.Sheria ipo na lazima ifuatwe. Wakati huo huo Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam amesema Mihadhara yote ya kidini kwa sasa
imesimamishwa kwa kipindi hiki kigumu mpaka hapo hali itakapokuwa
shwari. NAYE SHEIKH WA MKOA WA DAR ES SALAAM- Sheikh Alhadi Mussa
amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuwa na subira katika kulitatua
suala hili na wasijipange kufanya vurugu ya aina yoyote kwani suala hilo
limeshafika katika vyombo vya sheria hivyo tuviachie vyombo hivyo
vifanye kazi yake na haki itakuja kujulikana. Aidha Sheikh huyo
amesema kuwa ameridhishwa na maneno ya maaskofu katika kuwataka waumini
wao kuwa na utulivu na si kulipiza kisasi kwani.Lakini pia amewataka
waislamu nao watulie katika hilo. NAYE PADRI ANTHONY MAKUNDE –Katibu
Mkuu wa Balaza la Maaskofu(Tech) amesema kuwa anaungana na viongozi
wengine wa makanisa katika kuwasisitiza viongozi wa Dini ya Kikristo
kuendelea kuwa na subira katika kipindi hiki kwani njia pekee na sahihi
ya kutafuta suluhu na amani ni njia ya mazungumzo. KWA UPANDE WA
KAMANDA WA POLISI WA MKOA WA DAR ES SALAAM- Suleimani Kova amesema
kuwa Jeshi la Polisi limeungana na Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
katika kukabiliana na vurugu zitakazojitokeza katika Mkoa wa Dar es
Salaam.Aidha mtu yeyote akifanya kosa anachukuliwa kama mharifu kwa
sababu sheria haibagui wala kuchagua yenyewe inakata kotekote haiangalii
kama ni Padri au Sheikh. Kuhusu maandamano hayo yaliyopangwa Kamanda
kova amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vema katika kukabiliana na
hilo hivyo mtu yeyote akitaka kuandamana ajitahidi kutafakari mara
mbili mbili itakuwaje baada ya hapo kwa yeye na familia yake. Mwisho
kabisa kamanda Kova amewataka watu hawa wajisalimishe wenyewe kwa jeshi
la polisi ama sivyo sheria itachukua mkondo wake. -Mukadam Salehe -Kondo
Juma -Saaban Mapeo -Jaffary Mneke -Rajabu Katimba -Amani Moshi
إرسال تعليق