TAARIFA SAHIHI DHIDI YA UVUMI KUHUSU WANAFUNZI WANAOENDELEA KULAZIMIKA KUJAZA TENA TAARIFA ZAO ZA MIKOPO YA ELIMU YA JUU
Kumekuwa na uvumi kwamba mtandao wa
uombaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (OLAS)
ulikuwa na hitilafu ya kiufundi na hivyo Wanafunzi wanaondelea na masomo
ambao walikuwa tayari wameshahakiki taarifa zao wanapaswa kurejea
kujaza upya ama kuhakiki iwapo taarifa zao zipo mtandaoni.
Bodi inatumia fursa hii kuwajulisha Wanafunzi
husika, Vyuo vya
Elimu ya Juu na Umma kwa ujumla kuwa taarifa za
Wanafunzi hao zilizopokelewa ziko salama na hawapaswi kujaza tena na
hivyo taarifa hizo za uvumi zipuuzwe.
Aidha Bodi inasisitiza kwamba kesho tarehe 31
Julai, 2013 ni mwisho wa kupokea maombi ya mikopo ya waombaji wote
wanaotarajia kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo
2013/2014 na wale wanaoendelea na masomo na kwamba hakutakuwa na muda wa
nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.
Bodi inawapa nafasi ya mwisho waombaji wapya na
wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao hawajaomba mikopo kwa njia ya
mtandao, kuhakikisha wanatumia muda uliobaki kukamilisha taratibu zote
za maombi kupitia anuani ifuatayo: http://olas.heslb.go.tz au kupitia tovuti: www.heslb.go.tz
Tangazo hili limetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
إرسال تعليق